The House of Favourite Newspapers

Shirika La Amend Laendesha Mafunzo Ya Usalama Barabarani Na Huduma Ya Kwanza Kwa Bodaboda

0

Shirika la Amend kupitia ufadhili wa ubalozi wa Uswizi wanaendesha mafunzo ya usalama barabara ikiwemo huduma ya kwanza kwa madereva wa bodaboda zaidi ya 500 katika mkoa wa Tanga.

Wakiongea mara baada ya mafunzo hayo bodaboda wa Kata ya Magaoni na Mabawa katika Jiji la Tanga walisema kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia kujua umuhimu wa matumizi ya alama za barabara.

Mmoja wa bodaboda hao, Rehema Rashid alisema kuwa mafunzo yameweza kuwa mkombozi katika shughuli zake za kusafirisha abiria kwani awali hakuna na ufahamu wowote ule.

“Nilikuwa naendesha pikipiki lakini sijui lolote lakini baada ya mafunzo haya naelewa hata nikiwa barabara najua kitu Cha kufanya Ili kuzuia ajali na kuhakikisha nakuwa salama muda wote”alisema Rashid.

Kwa upande wake Afisa Miradi wa Taasisi ya Amend, Ramadhani Nyaza alisema kuwa mradi huo kwa ujumla wake umelenga kuwafikia zaidi ya madereva wa bodaboda 750 waliopo katika mikoa ya Tanga na Dodoma.

Alisema kuwa kwa mkoa wa Dodoma wameweza kuwafikia madereva 250 ambapo Kwa mkoa wa Tanga wanatarajiwa kuwafikia 500.

“Kulingana na takwimu za ajali kuonyesha kundi la bodaboda ndio lipo hatarini hivyo tumeona ni wakati Sasa wa kuendelea mafunzo hayo Ili kupunguza ajali lakini na kuwalinda madereva hao ambao kundi kubwa ni vijana”alisema Nyanza.

Hata hivyo Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mikanjuni Rehema Saidi aliwataka vijana kujitokeza Kwa wingi kupata elimu ya usalama wa barabara na jinsi ya kuendesha chombo Kwa usalama na kuepuka ajali.

“Elimu hii ninzuri sana hususani Kwa vijana wetu wanaofanya shughuli ya usafirishaji kwani ni bure lakini itaweza kuwasaidia na kuwaepusha na ajali ambazo zinaepukika”alisema Said.

Leave A Reply