The House of Favourite Newspapers

Alichokisema Mourinho baada ya kutangazwa rasmi Man U

0
Kocha mpya wa Man United, Jose Mourinho amesema maneno kadhaa mara tu baada ya kukabidhiwa kikosi hicho kwa kutangazwa mbele ya waandishi.
Katika shughuli hiyo ya kutangazwa jana, Mourinho alisisitiza suala la kuhakikisha Man United inakuwa timu inayofuzu kwa uhakika kucheza michuano ya kimataifa hasa Ligi ya Mabingwa.
Lakini amesisitiza atakuwa ni mtu mwenye kufanya maamuzi magumu bila ya uoga.
Kilichowavutia wengi, ni baada ya Mourinho kusema anahitaji kila kitu na kama inawezekana ni kushinda mataji yote.
 
TAKWIMU:
UMRI: 53
CLUB ALIZOFUNDISHA:
2000 Benfica
2001-02 Uniao de Leiria
2002-04 Porto
2007-07 Chelsea
2008-10 Inter Milan
2010-13 Real Madrid
2013-15 Chelsea
2016-present Manchester United
Honours:
Champions League x2
UEFA Cup x1
Premier League x3
FA Cup x1
League Cup x3
La Liga x1
Spanish cup x1
Serie A x2
Italian cup x1
Portuguese league x2
Portuguese cup x1
Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United, lakini akaonekana pia kumkejeli meneja wa Arsenal Arsene Wenger.

Amesema ”niko mahala nitakapo”.

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ”Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata”.

Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea, alijibu, akionekana kumrejelea Wenger: ”Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita. Wengine bado kabisa. Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita”.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo mwezi Mei.

Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.

Nataka kila kitu,alisema.Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono. ”Ni kweli hatuwezi kupata kila kitu, lakini tunataka”.

Leave A Reply