The House of Favourite Newspapers

92 Wafariki kwa Virusi vya LASSA

0

WATU 92 raia wa Nigeria wamefariki kuanzia Januari 2021 mpaka sasa kutokana na virusi vya Lassa. Taarifa zinaeleza kua majimbo ya Bauchi na Ebonyi yanaongoza kwa kuwa na virusi vipya.

Taarifa hiyo imetolewa Jumanne Disemba 28, 2021 na kituo cha kudhibiti magonjwa (NCDC) huku watu wawili wakipoteza maisha katika Jimbo la Bauchi na mmoja Jimbo la Ebonyi.

“Kwa jumla kutoka wiki ya kwanza hadi Wiki ya 50, 2021, vifo 92 vimeripotiwa na kiwango cha visa ni asilimia 20.3, ambacho ni cha chini kuliko kipindi kama hicho mnamo 2020 ambapo ni asilimia 20.7,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Wakala wa Habari Nigeria (NAN) imeeleza kuwa Taifa hilo limeendelea kuripoti visa na milipuko na ugonjwa huo unazidi kuwa janga katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi kama vile Jamhuri ya Benin, Ghana, Mali na eneo la Mto Mano (Sierra Leone, Liberia na Guinea).

Leave A Reply