The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Marufuku Kuwapa Biashara Watoto

0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema jukumu la kulea watoto na kutafuta mahitaji ni la wazazi lakini wajibu wa kuwasomesha watoto hao ni la serikali na kwamba ni marufuku kuwatumikisha watoto biashara.

“Tulishasema, mtoto wa Kitanzania kwenda shule ni lazima. Watoto ni wao, lakini kwenda shule ni lazima. Ndiyo maana serikali ilifuta ada katika shule zote.” amesema Majaliwa akizungumzana viongozi wa mkoa wa Lindi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, mkoani humo.

“Tunataka tuondoe kabisa tabia ya kukuta watoto wetu wakifanya biashara kwenye stendi za mabasi au nyumba za starehe,.” amesema.

Amesema ujenzi wa madarasa unaoendelea kote nchini hivi sasa, unalenga kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anakwenda shule iwe ni ya msingi au ni ya sekondari.

Leave A Reply