The House of Favourite Newspapers

Wananchi Washauriwa Kutembelea Vituo vya Hali ya Hewa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo.
Baadhi ya wanahabari wakichukua matukio hatika hafla hiyo.

Na Denis Mtima/GPL

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imewaomba wananchi kutembelea vituo vya hali ya hewa ili kuona shughuli zinazotolewazo na mamlaka hiyo na kujifunza.

Hayo yamesema leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Agnes Kijazi, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani ambalo lina wanachama 191.

Kijazi alisema mamlaka kwa upande wake hutembelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbalimbali nchini kupitia ofisi zake zilizopo nchi nzima.

Kaulimbiu ya siku ya maadhimisho hayo ni: ”Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake”.

 

Comments are closed.