The House of Favourite Newspapers

Yanga Kuna Kombinesheni 3 Hatari

0
Wachezaji wa Yanga wakipasha.

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina ameonekana kutengeneza safu mbili za ushambuliaji atakazozitumia kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 26, mwaka huu.

Kocha huyo raia wa Zambia, alionekana kutengeneza pacha hizo mbili za kufumania nyavu kwenye mchezo kirafiki juzi Jumamosi dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Katika mechi hiyo, mabao ya Yanga yalifungwa na Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin huku ya Singida yakipachikwa na Danny Usengimana na Simbarashe Nhiri.

Lwandamina katika kikosi cha kwanza ambacho alikianzisha aliwapanga washambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma aliyecheza namba 9 na Ibrahim Ajibu aliyecheza namba 10.

Washambuliaji hao, walionekana kucheza kwa kuelewana kutokana na kuchezeshana kwa maana ya kupigiana pasi za kufunga mabao katika mchezo huo ambao ulimalizika bila ya wachezaji hao kufunga mabao.

 

Licha ya wachezaji kutoelewana lakini viungo, Raphael Daudi aliyekuwa anacheza namba 8 na Pius Busitwa aliyecheza namba 11 walionekana kuwachezesha vizuri washambuliaji hao.

Ajibu na Ngoma walishindwa kuwa tishio kwenye lango la Singida kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo hawakuwapa nafasi ya kumiliki mipira.

Katika kipindi pili cha mchezo huo, Lwandamina alifanya mabadiliko kidogo kwenye safu ya ushambuliaji kwa kumtoa Busitwa na nafasi yake kuchukuliwa na Tambwe huku akimtaka Ajibu ahamie kucheza pembeni namba 11.

 

Ajibu alipopelekwa pembeni, Tambwe akaingia ndani kucheza nafasi yake pamoja na Ngoma yaani namba 9 na 10, hiyo yote katika kutengeneza pacha nzuri itakayocheza kwa kuelewana.

Dakika chache baadaye, Ngoma alitolewa na kuingia Emmanuel Martin aliyekwenda kucheza namba 7 na baadaye Lwandamina alimuhamishia kati Juma Mahadhi kucheza namba 9 huku Tambwe akicheza 10.

 

Mabadiliko hayo, yalionekana kuipa uhai Yanga ambayo ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini waliweza kutoka nyuma na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Tambwe aliyefunga kwa penalti na baadaye Martin kufunga la tatu.

 

 Wilbert Molandi | CHAMPIONI | Dar es SalaamIbrahim Mressy | Dar es Salaam

Leave A Reply