The House of Favourite Newspapers

MKAZI WA IRINGA AKABIDHIWA  NDINGA YAKE NA TBL

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja  wa TBL, David Tarimo (wa tatu kulia) akimkabidhi kadi mshindi wa gari, Frank Nathan,  ambaye ni mkazi wa Iringa.
Frank Nathan na mkewe (kulia) wakiangalia nembo ya TBL iliyoko kwenye gari hilo.

 

 

KAMPUNI ya bia nchini (TBL) leo Desemba 13 imemkabidhi mshindi wa pili wa zawadi kubwa ya gari  aina ya Renault KWDI, Frank Nathan,  baada ya kutangazwa wiki iliyopita kuwa mshindi wa droo ya promosheni inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga”.

 

TBL ilizindua promosheni hiyo inayojulikana kama ‘TBL kumenoga,Tukutane baa’ kwa lengo la kuwashukuru wateja wake na inafanyika kwenye baa mbalimbali nchini  ambapo washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI kwa kila mshindi wa droo kubwa ya mwezi na promoheni itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia ilipozinduliwa miezi miwili  iliyopita.

 

 

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja TBL, David Tarimo, amesema promosheni hiyo itafanyika kupitia chapa maarufu za bia zinazozalishwa na kampuni ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 

Kwa upande wake, Frank Nathan, ambaye ni mshindi katika promosheni hiyo amepongeza Kampuni ya TBL kwa kuendesha shindano hilo kwani hakutegemea kama angeliweza kujishindia gari hiyo.

 

Vilevile,  mbali na zawadi kubwa ya gari zipo zawadi nyingi za kujishindia kupitia promosheni hiyo ikiwemo bia za bure na kwamba  promosheni hiyo itakuwa inafanyika wikiendi ambapo kila sehemu ya promosheni kutakuwepo bendera ya TBL Kumenoga.

 

Alisema ili kushiriki promosheni hiyo ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ anachotakiwa kufanya mteja ni kununua bia tatu za chapa zilizopo kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia simu zao za mkononi kwenda namba 15451 kwa kutumia mitandao ya simu ya makampuni ya Vodacom, Tigo na Airtel. Wateja wenye mitandao mingine ya simu wanaweza kushiriki promosheni kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.tz.

Comments are closed.