The House of Favourite Newspapers

Makambo Afunika Rekodi Ya Okwi Bara

Heritier Makambo wa Yanga

STRAIKA Heritier Makambo wa Yanga hivi karibuni alivunja rekodi yake aliyoiweka ya kufunga mabao saba katika kipindi cha kwanza kwenye kila mechi za timu hiyo baada ya kufunga bao kipindi cha pili na kuifanya Yanga iibuke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United.

 

Makambo ambaye sasa ana mabao nane aliandika rekodi ya kufunga mabao saba katika kipindi cha kwanza tena huku akiwa ndiye mtu wa kwanza kufanya hivyo.

 

Hii ni rekodi ya mchezaji huyo ambayo imewashinda mastaa kadhaa akiwemo Emmanuel Okwi wa Simba ambaye amecheza ligi hii kwa zaidi ya miaka sita.

 

Kwenye mchezo huo dhidi ya Biashara United uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, Makambo alifunga bao lake katika dakika ya 80 likiwa ndiyo la kwanza anafunga kipindi cha pili tangu ametua nchini.

 

Pia katika mchezo huo Makambo alishindwa kuendeleza rekodi yake ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la kwanza baada ya beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuwa ndiye mchezaji wa kwanza kupachika bao la kwanza.

 

Makambo alifunga mabao yake kipindi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Coastal Union, Lipuli FC, JKT Tanzania, Alliance Schools, Kagera Sugar, Mwadui FC.

Comments are closed.