The House of Favourite Newspapers

Wateja wa Halotel kupiga simu, kutumia intaneti bila kikomo

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nauyen Van Trung (mbele mwenye mvinyo) akimmiminia shampeni msanii maarufu Mr. Blue (wa pili kulia) kinywaji hicho kabla ya kugonganisha glasi hizo kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel, ‘Royal Bundle’ na ‘Tomato Bundle’ zilizofanyika leo Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam. 
Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nauyen Van Trung akizungumza jambo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel, ‘Royal Bundle’ na ‘Tomato Bundle’.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nauyen Van Trung (wa tatu kulia) akifurahiya jambo. 
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel.
Sehemu ya wageni maarufu wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel.
…Mhina Semwenda (wa pili kulia) akizungumza jambo na Afisa Uhusiano wa Halotel, Stella Pius kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel, ‘Royal Bundle’ na ‘Tomato Bundle’ 

 

Katika kuendeleza ubunifu wa kuwahudumia wateja kwa kuwapatia kile wanachokihitaji, kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imekuja na huduma ya ‘ROYAL BUNDLE’ ambayo itawawezesha wateja wake kupata huduma zisizo na kikomo kama vile kupiga bila kikomo simu za ndani na kimataifa, kutumia intaneti bila kikomo pamoja na kuunganishwa moja kwa moja pindi vifurushi vitakapokwisha.

 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung amesema kuwa mbali na kuzingatia ubora na unafuu wa huduma zao, ubunifu ni silaha kubwa ambayo wanaitegemea katika kuwafikia wateja wa makundi yote katika kila kona ya nchi.

 

“Ninayo furaha kubwa kuwatangazia ujio wa huduma hii kabambe ambayo italeta mapinduzi makubwa nchini. ‘ROYAL BUNDLE’ imekuja kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatamani kutumia huduma zetu bila ya kupata bugudha ya aina yoyote zikiwemo salio kuisha au intaneti kukata.

 

Tunatambua umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shughuli za kiuchumi hivyo tusingependa kampuni yetu kuwa kikwazo katika kulifanikisha hilo. Ndiyo maana leo tunawatangazia watanzania wote kuwa kwa shilingi 10,000 tu unaweza kupiga simu za ndani na kimataifa kama vile kwenda nchi za India, China, Canada na Marekani bila ya kikomo, kutumia intaneti bila ya kikomo, kutuma SMS bila ya kikomo, na kama haitoshi, mara tu muda wa kifurushi utakapokwisha tutakuunganisha mara kwa mara,” alisema Bw. Van Trung.

 

“Kama nilivyosema awali, huduma hii inawalenda wateja ambao hawapendi bugudha katika mawasiliano. Hii ni fursa pia kwa wateja ambao tayari wamekwishasajiliwa na Halotel, wakati kwa wateja wapya wao wataungwa moja kwa moja kwa gharama niliyoitaja awali bila ya kuweka salio.

 

 

Faida ni nyingi za kujiunga na huduma hii. Kwa mfano, kwa shilingi hiyo hiyo 10,000 kwa mwezi mteja atajipatia muda wa maongezi wa dakika 520 kupiga simu mitandao yote, kifurushi cha intaneti yenye kasi cha GB 2, pamoja na kuwezeshwa SMS 500.  Endapo kifurushi hiki kitafikia ukomo, mteja ataweza kuwasiliana kwa gharama nafuu kabisa. Ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa shilingi 1 tu, atatumia shilingi 2 tu kwa sekunde kupiga simu kimataifa, atajipatia MB 1 kwa shilingi 5 tu, na kutuma SMS kwa shilingi 2 tu. Kiufupi ukiwa na ‘ROYAL BUNDLE’ hakuna huduma yenye ukomo, ” alisisitiza Mkurugenzi wa Halotel nchini.

 

“Mteja ana uhuru wa kuchagua kuunganishwa moja kwa moja na huduma hii, lakini pia itajumuishwa na vifurushi vilivyobakia alivyojiunga awali au kuamua kujiunga mwenyewe kulingana na uhitaji wake katika mawasiliano,” alisema na kuhitimisha Bw.Son kuwa, “Tunaamini katika ubunifu kila kukicha ili kuweza kuyafikia makundi yote ya wateja wetu, wa mijini na vijijini. Tunatambua wateja wetu wanapenda huduma zenye ubora wa hali ya juu, nafuu na zenye uhakika. Tunawaahidi kuendelea kulitimiza hilo kama kauli mbiu yetu ili kusukuma gurudumu la shughuli za uchumi.”

 

Aidha, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuzindua huduma nyingine ya “TOMATO Bundle” ambayo ni maalum kwa wateja wa Halotel nchi nzima, itakayowawezesha kupiga simu BURE kwenda namba yoyote ya Halotel kwa dk 5 za MWANZO kwa KILA SIMU pamoja na kupata salio la ziada la bure la Sh4000 ambalo mteja atalitumia kwenye huduma nyingine za Halotel (Kwa Mwezi mzima).

 

“Ninayo furaha tena kuwatangazia ujio wa huduma nyingine samba samba ya “TOMATO BUNDLE” Ili Mteja aweze kufurahia huduma hii inapaswa awe na Laini ya Halotel ya Tomato ambayo atainunua kwa Sh8000 tu laini hiyo itamuwezesha’ Kupiga simu kwa kila namba yoyote ya Halotel bure kwa dakika 5 za mwanzo, licha ya hapo mteja atapata salio la ziada la Tsh, 4,000 bure, ambalo atalitumia kwenye huduma nyingine apendazo za Halotel” Ili kuweza kujua salio hilo la ziada, mteja atapiga *102#. Alisema na kuongeza Trung.

Comments are closed.