The House of Favourite Newspapers

Azam yawavizia Ngoma, Tambwe

0

SIMBA YANGA (12)Martha Mboma, Dar es Salaam

IKIWA imebaki wiki moja tu ili Yanga icheze na Azam FC mechi ya Ligi Kuu Bara, mabeki wa Azam wameanza kufuatilia mbinu za mastarika Donald Ngoma na Amissi Tambwe ili wasilete madhara.

Aggrey Morris ni beki mkongwe na mwenye nguvu kikosini, akiwa na Pascal Wawa kwa pamoja wanautumia muda huu wa mapumziko kutazama video za mechi za Yanga ili kujua ni jinsi gani watawazuia Ngoma na Tambwe.

Katika ligi kuu, msimu uliopita timu hizo zilipokutana awali zilitoka sare ya mabao 2-2, ziliporudiana Yanga ilifungwa mabao 2-1 katika mechi iliyokosa ushindani wa kweli.

Morris aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Tunaendelea kujifunza mbinu mpya zaidi ili kukabiliana nao (Ngoma na Tambwe), msimu huu hatutaki kurudia makosa.

“Tutakuja na mbinu mpya za kuwazuia kwani tunautumia vizuri muda huu wa mapumziko ya mechi za kimataifa kuwasoma wao.”

Mabeki wengine wa Azam ni Said Morad, Shomari Kapombe na Gadiel Michael.

Leave A Reply