The House of Favourite Newspapers

MALAWI WAPIGA KURA KUCHAGUA RAIS NA WABUNGE

Wananchi wa Malawi leo Jumann, Mei 21, 2019 wampiga kura kuchagua Rais na wabunge baada ya kampeni zilizokuwa na ushindani mkali.

Wapiga kura Milioni 6.8 wameshiriki katika Uchaguzi huo, huku nusu wakiwa ni vijana na ushindani mkubwa ukiwa kati ya Rais wa sasa, Prof. Peter Mutharika, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2014, akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa naibu wake Dkt. Saulos Chilima na mhubiri wa zamani wa Lazarus Chakwera.

Mutharika kuwania muhula wa pili kumejikita katika ajenda ya uchumi na rekodi zake za kuimarisha miundombinu za barabara na umeme katika eneo la kusini mashariki mwa nchi.

Chini ya utawala wa Mutharika, mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 23 hadi chini ya asilimia tisa, lakini bado asilimia 11 tu ya watu ndio wanapata umeme.

Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu kuanzishwa sheria mpya inayohimiza vyama kutangaza mchango mkubwa na kupiga marufuku mazoea ya wagombea wa kutoa fedha kwa raia.

Comments are closed.