The House of Favourite Newspapers

Walichokifanya Airtel, Hakijawahi Kutokea, Unapiga Mitandao Yote? – Video

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam baada ya Airtel kuzindua huduma mpya ya ‘TAMBA MITANDAO YOTE’. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda.

 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa wateja wake huduma kabambe na za kipekee ikiwa ni jibu na itikio la mahitaji  ya wateja wao kwa kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’. Huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando.

 

TAMBA MITANDAO YOTE inakuja wakati muafaka na kuwapa wateja wa Airtel uhuru wa kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa punguzo la kiasi cha Tsh 1 kwa kila sekunde hata kama mteja hajajiunga na bando au kuishiwa bando.

 

Mkurugenzi wa Masoko Airtel, Isaack Nchunda akizungumza juzi Jumatano, Mei 22, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua TAMBA MITANDAO YOTE kwa niamba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema; ‘Tunayo furaha kubwa kuzindua huduma hii ambayo inawapa wateja wa Airtel uhakika wa kupiga simu kwenda mtandao wowote hapa nchini kwa gharama nafuu ya Tsh 1 kwa sekunde, tunaamini kupitia Tamba Mitandao Yote  mteja wetu  ataona thamani ya pesa yake na kufurahia uhuru wa kuongea wakati wowote.”

 

Nchunda aliongeza kuwa wateja wa Airtel watafurahia pia punguzo la vifurushi vya intaneti kutoka Tsh 172 kwa MB mpaka Tsh 40 kwa MB ikiwa hajajiunga na bando lolote,  pia mteja atafurahia kutumia Tsh 10 tu kwa MB ikiwa mteja alikuwa na kifurushi cha bando ambacho hakijaisha muda wake huku punguzo la gharama za ujumbe mfupi zikishuka kutoka  Tsh 69 kwa kila ujumbe mpaka Tsh 10 kwa kila ujumbe’.

Singano na Nchunda wakionyesha bango baada ya ya Airtel kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’.

 

 ”TAMBA MITANDAO YOTE” ni huduma ambayo inampa mteja wa Airtel huduma bora, huru na nafuu, hata kama atakuwa hajajiunga na bando yoyote bado anaweza kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa gharama ndogo ya Tsh 1 kwa sekunde. Tunaamini hii ni hatua kubwa sana kwenye sekta ya mawasiliano ambapo vikwazo vyote vimeondolewa na kuwapa Watanzania unafuu wa kupiga simu bila kujali kipato chake,’ alisema Nchunda.

 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano alisema ‘Kulingana na taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya wateja wanaotumia simu za mkononi kwa kupiga kati ya mwaka 2017 na 2018 imeongezeka kutoka milioni 40 mpaka milioni 43.

 

Idadi ya wateja wetu imeongezeka pia kwa kipindi cha robo mbili za mwaka uliopita na hii imetokana na  hudumu zetu zenye ubunifu na unafuu wa hali ya juu. Tunaamini huduma yetu itawawezesha wateja wetu kupata uhuru wa kupiga na kuongea ,wakiokoa fedha zao na kuziweka kwenye maendeleo ya kiuchumi.

 

Airtel imekuwa mstari wa mbele kwenye kuleta huduma nafuu na zenye ubunifu ambazo zinakidhi matakwa ya wateja wetu kama vile huduma za kifedha, SMS, kupiga simu na hata kwenye huduma za intaneti.

 

‘Airtel inaendelea kukuza wigo wa mtandao wake nchini ambapo kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money Branches zaidi ya 650 ambapo mteja anaweza kupata bidhaa na huduma mbalimbali kama za kifedha, kuunganisha kwenye vifurushi vya intaneti pamoja na kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole’, aliongeza Singano.

 

AIRTEL WAJA NA MPYA!! Tamba Mitandao Yote…

Comments are closed.