The House of Favourite Newspapers

Bao la Ngoma lamkuna Pluijm

0

DONALD NGOMA

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

LICHA ya timu yake kutoka sare ya bao 1-1 na Azam FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amelisifu bao la mshambuliaji wake, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Mshambuliaji huyo, alifunga bao hilo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa juzi Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao hilo ambalo ni la tano kwa mshambuliaji huyo kwenye ligi kuu, alilipachika akiunganisha krosi safi ya Juma Abdul kabla ya kukontroo mpira kwa kuutuliza kifuani kabla ya kuruka tik tak safi na kufunga kwenye ‘engo’ ya pembeni kabisa na kumuacha kipa Aishi Manula akiwa hana la kufanya.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Pluijm alisema kuwa bao hilo la mshambuliaji huyo limeingia kwenye orodha ya mabao mazuri yaliyofungwa kwenye timu hiyo.

Pluijm alisema mshambuliaji huyo anastahili pongezi nyingi kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha wa kukontroo mpira ukiwa juu kwa kifua kabla ya kufunga bao hilo.

Aliongeza kuwa, bao hilo alilolifunga ni kutokana na juhudi binafsi, hiyo yote ni katika kuhakikisha anatimiza majukumu yake.

“Bao alilolifunga Ngoma ni ‘fantastic’, kiukweli anahitaji pongezi ya hali ya juu kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha. Pia nampongeza aliyepiga krosi ya bao hilo ambaye ni Abdul, kabla ya kupiga alinyanyua uso wake na kumtazama Ngoma na kupiga krosi iliyomfikia na kufunga,” alisema Pluijm.

Leave A Reply