The House of Favourite Newspapers

JPM Awapa Fedha Majeruhi wa Morogoro, Kutibiwa na Serikali – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya Lori la Mafuta kupinduka na kuteketea kwa moto.

RAIS  Magufuli  leo Agosti 11, 2019 amewatembelea majeruhi 43 wa ajali ya moto iliyotokea jana mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuwapatia kila mmoja Sh500,000 kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati alipokuwa akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto ambao wameletwa kutoka mkoani Morogoro kwa ajili ya matibabu.

Ajali hiyo ilitotokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika mtaa wa Itigi, Msamvu mkoani Morogoro mita 200 kabla ya kufika kituo cha mabasi cha Msamvu barabara ya Morogoro- Dar es Salaam baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Rais  Magufuli akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto ambao wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kusafirishwa kutokea mkoani Morogoro.

Majeruhi 46 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walihamishiwa MNH. Hata hivyo, watatu kati yao wamefariki dunia leo.

Akiwa katika wodi ya Sewahaji na Mwaisela, alizungumza na majeruhi hao kuwashukuru wauguzi pamoja na madaktari kwa huduma nzuri na kuwazawadia Sh1 milioni.

Rais  Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kutoka kuwajulia hali majeruhi.
Rais wa  Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kitengo cha Dharura na kuelekea katika Wodi za Wagonjwa kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto.

 

Comments are closed.