The House of Favourite Newspapers

PROF. NDALICHAKO AWATAKA WALIMU KUJIWEKEA AKIBA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Banki Plc, Bw. Richard akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Kigoma wakifuatlia hotuba ya Waziri Ndalichako wakati akifunga kongamano la walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Walimu Kasulu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiagana na Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Banki Plc, Richard  Makungwa.

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka walimu kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kwamba akiba huwekwa kabla ya matumizi.

 

 

Profesa Ndalichako ameyasema hayo wakati akihutubia Kongamano la “Amsha Amsha na Mwalimu Bnk” lililofanyika katika ukumbi wa Serengeti wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Septemba 14, 2019.

 

 

Kongamano hilo lililoandaliwa na Mwalimu Commercial Bank Plc limewaleta pamoja wawakilishi wa walimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Kigoma na lengo lake ni kutoa elimu ya fedha, lakini pia umuhimu wa walimu kuweka amana zao katika benki ya Mwalimu ambayo ilianzishwa kwa lengo la kutatua changamoto za kifedha kwa walimu.

 

“Nisingependa mwalimu apate matatizo ya kifedha kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya fedha, kwasababu yawezekana kuna matatizo ya kibenki lakini kuna matatizo mengine ambayo mwalimu anaeweza kuyapata kwasababu ya kukosa elimu ya fedha kwa hiyo naomba muendelee kutoa hiyo elimu fedha vizuri kwa walimu  na mimi nisisitize kwamba akiba ni kile kitu unachoweka kabla ya kufanya matumizi.” Alisema Profeesa Ndalichako na kuongeza.

 

“Matumizi kila siku hayataisha kwahiyo naomba sana walimu mjiwekee akiba yaweza ikawa shilingi elfu 10,000 kwa mwezi au elfu 30,000 kwa mwezi, maana haba na haba hujaza kibaba.” Alibainisha waziri huyo wa Elimu.

 

 

Alisema “Mwalimu Commercial Bank ni benki yetu, mimi mwenyewe ninahisa, benki yoyote ili ifanye vizuri inategemea idadi ya wateja na  kiwango cha uwekezaji katka benki husika, kwahiyo niwaombe sana walimu tuitumie benki hii.” Alisema.

 

 

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Banki Plc, Bw. Richard Makungwa alisema, benki imedhamiria kwa dhati kuwafikia wateja wake ambao ni walimu kote nchini ili kutoa hamasa ya ushiriki wa walimu kwenye benki yao ambayo ina miaka mitatu tangu ianzishwe.

 

 

“Ni matumaini yangu kwa idadi ya walimu ilivyo, benki hii itakuwa imara, nitoe wito kwenu ninyi walimu itumieni benki yenu kwa kuweka amana nah ii itawezesha kuwahudumia kwa lengo lililokusudiwa la kuondoa changamoto za kifedha kwa walimu kwani hii ni mali yenu.” Alisema Bw. Makungwa na kuongeza,…….tumeanza hapa Mkoani Kigoma na hii “Amsha Amsha na Mwalimu Bank” na tutaendelea kwenye mikoa mingine kwa lengo la kuhakikisha idadi kubwa ya walimu inatumia huduma za benki ya Mwalimu.” Alisisitiza Bw. Makungwa.

Comments are closed.