The House of Favourite Newspapers

Hospitali Kubwa Kanda ya Ziwa Kujengwa Chato

0

SERIKALI  ya Tanzania imesema ina mpango wa kujenga Hospitali ya Kanda ya Ziwa wilayani Chato mkoani Geita itakayohudumia wakazi wote waishio mikoa ya kanda hiyo.

 

Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jana Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema serikali inatarajiwa kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu katika eneo hilo.

 

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (Hospitali ya Kanda) Chato,” alisema na kuongeza kwamba sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni mikoa ya kanda hiyo kuwa  na watu zaidi ya milioni 15.

Leave A Reply