The House of Favourite Newspapers

Simba: Chama, Kanda Hawaendi Popote

0

KATIKA kukiboresha kikosi chao, uongozi wa Simba umeahidi kutomuachia mchezaji yeyote watakayemuhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu zienee tetesi za viungo wao, Mzambia Clatous Chama na Mkongomani, Deo Kanda saini zao kuwaniwa na watani wao wa jadi, Yanga.

Nyota kadhaa wa Simba mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu akiwemo Yusuf Mlipili, Hassani Dilunga, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim na Deo Kanda anayecheza hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe. Chama mkataba wake umebaki mwaka mmoja.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, uongozi wa timu hiyo umetenga fedha ili kuhakikisha wachezaji wanaomaliza mikataba yao Nyota kadhaa wa Simba mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu akiwemo Yusuf Mlipili, Hassani Dilunga, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim na Deo Kanda anayecheza hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe. Chama mkataba wake umebaki mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, uongozi wa timu hiyo umetenga fedha ili kuhakikisha wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu hawaondoki Simba katika kukijenga kikosi imara kitakacholeta ushindani kimataifa.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa wanaamini katika hilo watafanikiwa kutokana na kuwepo vizuri kiuchumi, hivyo mchezaji atakayeondoka ni yule ambaye hayupo kwenye mipango yao. Aliongeza kuwa tayari mazungumzo kati yao na Chama na Kanda yanakwenda vizuri.

 

“Uongozi unafahamu unachokifanya, hivyo hawana hofu juu ya wachezaji wanaotajwa kuwa wanaondoka mwishoni mwa msimu kutokana na mikataba yao kumalizika. “Tayari viongozi wamefanya mazungumzo na wachezaji wao wote wanaowahitaji kwa ajili ya kuwaongezea mikataba, lakini wale ambao hawapo kwenye mipango yao, wameachana nao.

 

“Kati ya hao yupo Mlipili na Mo Ibrahim ambao huenda ukawa msimu wao wa mwisho kuwa wachezaji wa Simba,” alisema mtoa taarifa huyo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema: “Kwa mchezaji tunayemuhitaji, hakuna atakayeondoka, tayari uongozi umeanza mazungumzo na baadhi ya wachezaji wanaomaliza mikataba yao.

Huyu MORRISON Ni HATARI, Afanya MAZOEZI Nyumbani, LIGI Ikianza MMEKWISHA..!

Leave A Reply