The House of Favourite Newspapers

Ntibazonkiza Afunguka Alivyowatolea Nje Yanga

0

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza, amesema timu hiyo ilianza kumfuatilia miezi miwili hadi mitatu iliyopita kabla ya kufikia makubaliano ya kusaini mkataba huku akitamba ametua kwa kazi moja tu ya kusaidia timu kutwaa mataji.

 

Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga mapema Jumatatu iliyopita kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa mchezaji huru ambapo vijana hao wa Jangwani walimnasa baada ya kumalizika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Burundi uliomalizika kwa Burundi kupata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na yeye.

 

Kwa mujibu wa Ntibazonkiza amekiri ujio wake katika timu hiyo, kocha mpya Cedric Kaze amehusika kwa asilimia mia moja kutokana na kuwahi kumfundisha kwenye timu ya Taifa ya Burundi, mwaka 2011.“Mimi nimekuja Yanga sio kwa bahati mbaya, wapo wanaofikiria nimesajiliwa baada ya mchezo dhidi ya Tanzania.

 

Tulikuwa na mazungumzo na Yanga miezi miwili au mitatu nyuma.“Lakini nilishindwa kujiunga nao kutokana na changamoto kadhaa zilizokuwepo wakati huo. Sasa nilipokuja tena hapa ikawa rahisi kumalizana nao kwani hata yale yaliyotukwamisha mwanzo hayapo.

“Mara kwa mara nilikuwa nikiwasiliana na kocha Kaze (Cedric) kabla ya mpango wa kusaini Yanga haujafikia pazuri mimi kusaini mkataba, kabla ya kusaini kocha alinipigia simu na kunielekeza ananihitaji hivyo niwasikilize viongozi wa Yanga nimezungumza naye pia baada ya kusaini amenieleza mipango yake hapa,” alisema Ntibazonkiza.

 

Ntibazonkiza ataanza kuitumikia Yanga mwezi Desemba pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa lakini atakuwa na muda wa kuzoeana na wenzake kwani ataanza kujifua na mabingwa hao wa kihistoria Novemba 15, siku ambayo mkataba wake utaanza rasmi.

Wilbert Molandina Leen Essau

Leave A Reply