The House of Favourite Newspapers

TFF Yasaini Mkataba wa Kukuza Miundombinu ya Soka

0

SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF) limesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo ya kukuza miundombinu ya soka na Chuo cha Uhasibu Arusha.

 

Mkataba huo unalenga kuendeleza soka na miundombinu yake katika Viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha na katika menejimenti ya TFF ambapo pande zote mbili zimekubaliana.

 

Chuo hicho kitatoa udhamini wa mafunzo kwa asilimia 100 ya ada pamoja na malazi kwa wanafunzi ambao TFF itawatambua kama wanamichezo wanaostahili kupewa udhamini huo.

 

Aidha, chuo kitatoa msaada mkubwa katika malengo ya TFF ya kuanzisha shule ya uongozi wa soka na kuendeleza elimu kuhusu soka la wanawake.

 

Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utiaji saini alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa aliwapongeza TFF na Chuo cha Uhasibu Arusha kwa maono mazuri.

 

Naye, Rais waTFF, Wallace Karia alisema wanaenda na spidi ya kisayansi ambapo wanaongozwa na mpango mkakati ambao ni irani aliyoitumia wakati akiwania urais.

 

Naye mkuu wa chuo hicho, Profesa Eliamani Sedokeya alisema michezo kwa sasa ni biashara ndiyo maana wameingia mkataba huo.

Stori na Kennedy Lucas, Arusha | Championi

Leave A Reply