The House of Favourite Newspapers

Kili Marathon 2021 Yabadili Madhari ya Mji wa Moshi, Kufanyika kesho

0
Wakazi wa Mji wa Moshi Mkoa wa Kilimanjaro,wakiwa kwenye foleni yakuchukua namba za usajili wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni kati Kilomita 5,Kilomita 21 Kilomita 42,zinazo tarajia kufanyika kesho tarehe 28 mwezi huu, katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Zoezi hilo lilianza Alhamisi ,Ijuma na Jumamosi,litakapo fungwa zoezi hilo.

MJI wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, umekuwa kituo kikubwa cha shughuli nyingi kutokana na kuanza kuwasili mjini humo, washiriki wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa mwaka wa 2021 zinazotarajiwa kufanyika mjini hapo Jumapili ijayo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mbio za Kilimanjaro Premium Lager, John Bayo, maandalizi yote muhimu kuelekea siku ya tukio hilo yamekamilika, ambapo washiriki wanatarajiwa kushiriki katika mbio za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Full Marathon) na KILOMITA 5 zijulikazo kama Grand Malt 5 Km Fun Run.

“Kuelekea mbio hizi zinazotarajiwa kufanyika Februari 28, mwaka huu, ambapo washiriki wanatarajia kwa kuanzia na kumalizia katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), maandalizi yake yameshakamilika kwa asilimia 95”, alisema.

Bayo aliendelea kusema kuwa kamati ya maandalizi tayari imehakikishiwa uongozi wa jeshi la polisi mkoani humo usalama wa kutosha wakati wa mbio hizo.

“Pia tumepokea hakikisho kutoka kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhusu hali ya njia zitakazotumiwa, ambapo wamesema tayari wametoa vibali maalum vya kufunga barabara ambazo zitatumika wakati wa mbio”, alisema na kuongeza, siku hiyo barabara husika zitafungwa kutoka saa 12 asubuhi hadi saa saa 5 asubuhi.

Alizitaja barabara hizo kuwa ni barabara ya Sukari, inayoelekea kwenye kiwanda cha sukari cha TPC, npamoja na barabara ya Kilimanjaro, barabara ya Lema, barabara ya Sokoine, barabara ya Khambaita, barabara ya VETA na ile ya Bustani Alley.

Alisema kama sehemu ya maandalizi yanayoendelea washiriki bado wanaendelea kuchukua tiketi zao za ushiriki zoezi ambalo alisema linafanyika katika hoteli ya Keys, ambapo alisema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi siku moja kabla ya tukio lenyewe.

Akijibu maswali ya wanahabari, Bayo alithibitisha kuwa usajili wa ushiriki wa mbio za 42km na 5km bado unaendelea ila kwa washiriki watarajiwa kulipia kwa fedha taslimu na kwamba usajili wa mbio za 21km umefungwa baada ya tiketi zote kununuliwa.

Bayo pia alisisitiza kuwa waandaji wa mbio hizo zinazotarajiwa kushirikisha wakimbiaji kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea kutoa kipaumbele kwa tahadhari za kiafya ambapo alisema hatua hiyo ni kufuata miongozo yote ya kiafya inayotolewa na serikali.

Kwa upande wake Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi alisema kuelekea mbio hizo, wameandaa mfululizo wa matukio mwishoni mwa wiki na kwamba maandalizi yote kuhusiana na matukio hayo yanaenda vizuri.

“Tumeandaa matukio kadhaa Ijumaa na Jumamosi, ambapo kati ya matukio hayo ni burudani ambazo moja wapo itajumuisha onyesho la msanii wa Afrika Kusini Prince Kaybee ambalo limefanyika siku ya Ijumaa kwenye bustani zilizoko kwenye Hoteli ya Hugo”, alisema.

“Kilele cha shughuli na matukio yote haya ni siku ya Jumapili, wakati wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitakazofanyika kwenye Uwanja wa MoCU”, alisema.

Wakati huo huo hoteli nyingi na nyumba za wageni mjini Moshi tayari zimejaa Moshi kutokana na idadi kubwa ya washiriki ambao wanaendelea kuwasili mjini humo tayari kwa tukio hilo la Jumapili, ambapo maeneo mbalimbali ya kutoa burudani yameonekana kupaa wageni wengi.

Kwa upande wao wadhamini wa mbio hizo pia wameonekana wakifanya kila linalowezekana ikwemo kupamba maeneo mbalimbali ya mji kw aviashria vya kuweko kwa tukio hilo kubwa Afrika Mashariki na kusababisha msisimko mkubwa kwa wakazi wa Moshi na wageni.

Wadhamini wa tukio la la mwaka huu ni pamoja na, Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo – 21km Half Marathon, Grand Malt-5km, wadhamini wa meza za maji- Unilever Tanzania, Simba Cement, TPC Sugar, Kilimanjaro International Leather Company Limited, Kibo Palace Hotel na watoa huduma rasmi ni pamoja na Garda World, Keys Hotels na CMC motors.

Hafla hiyo imeandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions Limited.

Leave A Reply