The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atoa Msimamo wa Serikali Kuhusu Chanjo ya Corona – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali haitapokea kila ushauri unaotolewa hasa kuhusu masuala ya janga la Corona ikiwemo chanjo ya ugonjwa huo badala yake Serikali itajiridhisha kabla ya kuamua kutumia au kuacha.

 

Samia amesema hayo leo Ijumaa, Mei 14, 2021 wakati akihutubia Waislamu na Taifa kwenye baraza la Eid El-Fitr lililofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 

“Leo ni mara yangu ya kwanza kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid, lakini nawiwa vigumu kidogo kuzungumza mbele ya Masheikh na Maulamaa walio mbele yangu ila nitajitahidi.

 

“Nawasihi ndugu zangu Waislam, kuendeleza ucha Mungu tuliokuwa nao katika kipindi cha Ramadhani, usiishie jana baada ya mwezi kuandama. Tuendelee kutenda matendo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu na kujiepusha na yale yanayomchukiza Mungu, miongoni mwa matendo mema ni kufanya kazi kwa uadilifu.

 

“Napenda kuwasihi watumishi wa Serikali na Sekta Binafsi kuhakikisha wanafanya kazi na kupata kipato halali, wajiepushe na vitendo vya wizi, rushwa na urasmu. Niwasihi wafanyabishara walipe kodi stahiki kwa serikali.

 

“Nirudie kusisitiza umuhimu wa kila mmoja wetu kuendelea kuishi na matendo mema, na binafsi naamini endapo tutafanya hivyo baraka na Neema za Muumba tulizozipata wakati wa mfungo tutabaki nazo.

 

“Nawashukuru kwa kuwaasa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari za kinga na maambukizi ya Corona, ingawa mmetoa angalizo kuhusu suala la chanjo, kwahiyo hata suala la chanjo nalo tutajiridhisha kwanza kabla ya kuamua kutumia ama kuacha kutumia.

 

“Tahadhari mlizozitoa BAKWATA juu ya chanjo ya Corona zitafuatwa, Serikali yetu ila haina maana tutapokea kila tunacholetewa au kuambiwa lazima tujiridhishe, hata chanjo tutajiridhisha kabla ya kuamua kutumia au kuacha kutumia Watanzania msiwe na wasiwasi tuko makini,” amesema Rais Samia.

 

 

Leave A Reply