The House of Favourite Newspapers

TB Joshua Afariki Dunia – Video

0

MHUBIRI maarufu nchini Nigeria, Barani Afrika na Duniani kote, Nabii Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua ambahe ni mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) amefariki dunia jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini Nigeria.

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan inaeleza kwamba TB Joshua alifariki muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo Jumamosi.

TB Joshua alizaliwa mwaka 1963 na mpaka anakutwa na mauti alikuwa na umri wa miaka 58.

 

“Jumamosi Nabii TB Joshua alizungumza katika mkutano wa washirika kupitia Emmanuel TV alisema ‘kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada’.”


“Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia,” inaeleza taarifa hiyo.

 

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza chanzo cha kifo chake huku ikiwataka waumini kumwombea mhubiri huyo na kuwapa nafasi wanafamilia kuomboleza kifo cha mpendwa wao.

Advertisement

TB Joshua ni mwanzilishi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) na kituo cha televisheni cha Emmanuel TV ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake na kuwavutia watu wa mataifa mbalimbali.

 

Nabii huyo alikuja nchini mwaka 2015 wakati wa mbio za uchaguzi mkuu zikiwa zimepamba moto.

Alifanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa mgombea wa CCM, Hayati John Magufuli.

TB Joshua aliingia kwenye msukosuko mwaka 2014 baada ya kanisa lake kuporomoka na kuua watu na wengine kujeruhiwa.

Amefariki wakati kesi hiyo ikiwa bado inaendelea kwa mujibu wa chanzo kutoka Nigeria.

 


Taarifa zaidi kuhusu kifo chake tunakuleta hivi punde.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply