The House of Favourite Newspapers

Mama Ambariki Hamisa Kuolewa na Rick Ross

0

MAMA wa mwanamitindo na msanii-mjasiriamali maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga ameibuka na kusema kuwa hata siku moja hawezi kumchagulia au kumpangia mtu wa kumuoa mtoto wake huyo zaidi ya kumbariki.

 

Mama huyo anasema hawezi kuingilia uamuzi wa Mobeto kwa sababu ana uamuzi kwa kila kitu na yeye anasimama kama mama tu Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mama huyo anasema kuwa, anaona kwenye mitandao watu wengi wanamuuliza, vipi kuhusu mtoto wake kuolewa na Rick Ross; staa mkubwa wa muziki wa Marekani, kitu ambacho hawezi kukijibu kwa sababu ni maswali yanayomuhusu Mobeto mwenyewe.

 

“Ukweli ni kwamba mimi sina uamuzi wa kumchagulia Hamisa (Mobeto) mchumba wa kumuoa, kila kitu kiko mikononi mwake hivyo tumuachie mwenyewe na uamuzi wake

“Watu wasijali hata kidogo,” anasema mama huyo.Kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, habari inayotrendi ni mawasiliano ya Hamisa na Rick Ross; jambo ambalo watu wengi wanalitolea macho kuona uhusiano huo utakuwaje.

 

Mawasiliano ya Hamisa na Rick Ross yamefifisha zile tetesi kuwa, huwenda mrembo huyo anaolewa na mfanyabiashara maarufu Bongo, Fred Vunjabei ambaye ametangaza kufunga ndoa ifikapo Juni 16, mwaka huu.

Leave A Reply