The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya Miradi 21 ya Kilimo cha Umwagiliaji Yafufuliwa Nchini

0
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa

TUME ya Taifa ya Kilimo cha Umwagiliaji imefufua zaidi ya miradi 21 ya kilimo cha umwagiliaji katika mikoa mbalimabali iliyokuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu.

 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo Raymond Mndolwa alipokuwa akizungumza jana kuhusu mikakati iliyotumika kufufua miradi hiyo iliyokuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu, mikoa ambayo miradi hiyo imefufuliwa ni pamja na mkoa wa Morogoro, Iringa, Mbeya, Tabora pamoja na mkoa wa Mara.

 

Mkurugenzi huyo alisema kuwa vikwazo vilivyokuwa vinaikumba miradi hiyo sasa vimetatuliwa na kufanyiwa ufumbuzi.

Raymond Mndolwa akiwa pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

“moja ya changamoto ilikuwa ni Makandarasi, hivi sasa tayari miradi imepatiwa makandarasi wapya walioshinda zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo”

 

Mkurugenzi huyo pia aliwataka wataalamu wapya watakaokwenda kufanya kazi katika miradi hiyo kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuisaidia Serikali kuendelea katika sekta ya kilimo,alisema kwamba Serikali imetenga kiasi cha fedha bilioni 361 kwa mwaka 2022/23 kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hususani katika kilimo hivyo kuwataka wakulima kuchangamkia kilimo ili kuweza kujiinua kiuchumi.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao

Leave A Reply