The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Air Tanzania Yashindwa Kutua Katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba – Video

0

Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa.

Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ni Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Neema Lugangira ambaye baada ya tukio hilo, kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, aliandika ujumbe akielezea tukio hilo.

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Neema Lugangira.

 

Lugangira aliandika maneno yafuatayo:
“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar es Salaam. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba.”

“Abiria wengine wamebaki Mwanza, wengine tumerudi Dar salama. Airport ya Bukoba inajulikana kama airport yenye changamoto kijiographia na hali ya hewa ikiwa mbaya changamoto ya kutua inazidi. Nawapongeza Captain Emmanuel Msangi na 1st Officer Mhayyar Alnabhany kwa maamuzi sahihi.”

 

Global TV imezungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Tanzania, Mussa Mbura ambaye amesema ni kweli ndege hiyo kubwa imeshindwa kutua kutokana na ukungu uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Neema Lugangira akiwa katika picha ya pamoja na Marubani Emmanuel Msangi na 1st Officer Mhayyar Alnabhany.

 

Amesema watu wapuuze uvumi unaoendelea mitandaoni kwamba Uwanja wa Ndege wa Bukoba umefungwa kwani unafanya kazi kama kawaida.

 

Amesema kuwa, ni ndege kubwa tu za Air Tanzania na Precision Air ambazo hazitui kwenye uwanja huo, lakini ndege ndoa zinatua kama kawaida.

 

Leave A Reply