The House of Favourite Newspapers

Matajiri Yanga wamjadili Kiiza

2

kiiza-akishangilia-baada-ya-kutikisa-nyavu-uwanja-wa-taifa-dar-es-salaam_f9e7nzxc6j531t6oujg70lpkp  Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.

Wilbert Molandi na Khadija Mngwai
KASI ya kufunga mabao ya mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza inaonekana kuwa tishio kwa timu pinzani katika Ligi Kuu Bara lakini habari mpya ni kuwa baadhi ya mabosi wa zamani wa timu yake ya Yanga, wamekutana juzi usiku na lengo kuu likiwa ni kumjadili mchezaji huyo raia wa Uganda.
Kiiza ambaye alitemwa na Yanga mwaka juzi kwa madai ya kuwa ameshuka kiwango, yupo kileleni katika orodha ya wakali wa mabao akiwa na mabao 14, sawa na Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mmoja wa matajiri wa Yanga alisema walikutana wote kwa pamoja kwa ajili ya kujadili mwenendo wa timu yao kwenye mechi zilizobakia ili kuhakikisha wanatetea taji lao la ubingwa wanalolishikilia.

HAMISI-KIIZA-e1442762258493.jpg

…Akiongea na mashabiki zake baada ya kufunga bao katika moja ya mechi ya Ligi Kuu Bara.

Tajiri huyo alisema mbali na mwenendo wa timu yao, pia walimjadili Kiiza kutokana na kasi yake ya ufungaji tangu ametua kuichezea Simba mwanzoni mwa msimu huu.
Alisema walimchambua Mganda huyo na kwenda mbali zaidi kujadiliana juu ya mkataba wake na Simba.
Mkutano huo ulifanyika kwenye moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam na wamepanga kuendelea kukutana kwa ajili ya majadiliano zaidi.

kiiza.jpgWachezaji wa Simba wakishangilia pamoja na Kiiza.

“Kiiza hakuondolewa Yanga na viongozi, aliondolewa na benchi la ufundi ambalo ndilo lililokuwa na dhamana ya kuchagua wachezaji. Kiiza siyo mchezaji mbaya,” alisema tajiri huyo. Gazeti hili lilipowasiliana na Kiiza juu ya habari hizo na kumuuliza anazipokea vipi, alisema: “Sina taarifa zozote na nisingependa kulizungumzia hilo kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Simba na nina mkataba, akili yangu nimeielekeza kuitumikia klabu yangu.”

 

 

Kiiza aitangazia vita Yanga
Wakati huohuo, Kiiza amejinadi kuwa nia yao ni kuhakikisha wanashinda kila mechi bila kujali wanacheza wapi, hiyo ikiwa na maana hata Yanga ambao watakutana nao baadaye mwezi huu, maana yake kazi ni moja tu, kupata ushindi.
“Nashukuru kuona tunapata ushindi, nia yetu ni kushinda mechi zote zijazo,” alisema Kiiza.

2 Comments
  1. Global Publishers says

    Ngoja tusubiri mwisho wa majigambo.

  2. alex rodrick says

    simba katika ubora wake!!!!

Leave A Reply