The House of Favourite Newspapers

Airtel yazindua msimu wa pili wa Airtel Trace Music Stars‏

0

Pic 1.. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars litakalowapa nafasi watanzania kushiriki na kuonyesha vipaji vyao hatimae kujishindia zawadi nono ikiwemo kurekodi video na wimbo na mwanamuziki nguli wa Marekani , Keri Hilson. Pichani (Kushoto) Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza na (kulia) ni mshindi wa wa Airtel Trace Music Stars Afrika , Nalimi Mayunga

Pic 2..Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Beatrice Singano Mallya,( kushoto) na mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika , Nalimi Mayunga kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi msimu wa pili wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars nchini Tanzania

Pic 3 b..Pic 3..b

mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika , Nalimi Mayunga akiimba wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars litakalowapa nafasi watanzania kushiriki na kuonyesha vipaji vyao na hatimae kujishindia zawadi nono ikiwemo kurekodi video na wimbo na mwanamuziki nguli wa Marekani , Keri Hilson

 

 

Dar es Salaam, Jumanne 16 February 2016, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa pili wa shindano lake kubwa la muziki la Afrika la Airtel Trace Music Stars ambapo wanamuziki chipukizi nchini watapata nafasi yakuonyesha vipaji vyao ulimwenguni.

Msimu wa pili wa Airtel Trace Music Stars kwa mwaka huu utasimamiwa na nguli mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo ambae pia ni muigizaji maarufu Keri Hilson kutoka marekani

Shindano la Airtel Trace Music Stars msimu wa pili kwa mwaka huu litashirikisha nchi 9 barani Afrika zikiwemo Jamuhuri ya demokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Tanzania na Zambia

Mshindi kutoka katika nchi zinazoshiriki atapata nafasi ya kushiriki katika Mashindano ya Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika Lagos, nchini Nigeria mnamo mwezi Juni 2016.

Zawadi nono ya mshindi wa Afrika ni pamoja na mafunzo ya kuwa mwanamuziki bora kutoka kwa mwanamuziki nguli Keri Hilson ambapo yatafanyika Atlanta nchini Marekani, pamoja na kurekodi wimbo na mwanumuziki huyo. Mshindi hataishia kurekodi wimbo na Keri Hilson bali atapata nafasi ya kurekodi wimbo pamoja na walioimba wimbo wa “Knock You Down” na kusaini mkataba na kituo maarufu cha burudani cha Trace TV na kufanyiwa promosheni kwenye baadhi ya vipindi vyake

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Beatrice Singano Mallya alisema” Tunayofuraha kuzindua msimu wa pili wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars hapa Tanzania. Tunapenda kutoa wito kwa vijana wetu watanzania wenye vipaji kutoka katika maeneo mbalimbali kujitokeza na kushiriki katika mashindano haya. Tunaamini hili ni jukwaa la pekee litakalotoa FURSA na kuwawezesha vijana wengi kubadili maisha yao na kuzifikia ndoto zao katika tasnia ya muziki. Zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa shindano hili hapa Tanzania kwa mwaka huu ni kama ifuatavyo Milioni 50 kwa mshindi wa kwanza, million 3 na milioni 2 kwa washindi wa pili na watatu “.

Nae Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel Bi Prisca Tembo alifafanua jinsi ya kushiriki alisema “washiriki wanatakiwa kupiga namba 0901002233 kwa kutumia simu zao za mkononi na kurekodi nyimbo zao kwa gharama ya shilingi 150 tu kwa dakika ili kupata nafasi ya kuwa mwanamuziki bora Afrika. Baada ya kurekodi wimbo mshiriki atapata utambulisho wenye namba ambayo itawawezesha marafiki , ndugu , jamaa na wapenzi wa muziki wake kuweza kumpigia kura na kupata nafasi ya kushinda katika fainali za Tanzania na hatimae kushiriki katika mashindano ya Afrika. Kura zitapigwa kupitia ujumbe mfupi kwenda namba 15594 alieleza Prisca Tembo, Meneja huduma za ziada wa Airtel.

Mwaka Jana Airtel Trace Music Star ilifungua njia kwa mwanamuziki chipukizi Mayunga Nalimi na kumwezesha kuonyesha kipaji chake. Mayunga alishinda katika mashindano ya Afrika na kuzawadia na mwanamuziki nguli wa Marekani Akon kuwa mshindi wa Afrika. Nalimi alipata zawadi nono ikiwemo dili ya kurekodi nyimbo yake na studio ya Universal pamoja na kupata mafunzo na kurekodi wimbo wake na Akon nchini Marekani , zawadi zenye thamani ya $500,000

“Tunafurahi kwamba Mayunga amefanikiwa kurekodi wimbo wake wa kwanza wa “Nice Couple” ambao umekuwa ukiongoza kwa kuchezwa kwenye radio pamoja na TV nchini. Pamoja na mafunzo kutoka kwa Akon ujulikanayo kama “Please Don’t Go Away” ambao tunauzindua leo tunapozindua msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania”. alisema Tembo.

Leave A Reply