The House of Favourite Newspapers

Professor Jay: Sipendi kuitwa Mheshimiwa

0

PROF-JAY.jpg

Nguli wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Professor Jay’.

Hans Mloli
NGULI wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Professor Jay’ ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Mikumi, Morogoro amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake mapya ya ubunge kwa sasa lakini pia akagusia jinsi gani asivyopenda kuitwa mheshimiwa na muda gani ataendelea na kazi yake ya muziki.
Aidha, pia ameelezea fursa na nafasi nyingi anazozipata za kukamilisha mambo yake mapema baada ya kuwa na wadhifa huo kwa kuwa ana uwezo wa kuonana na watu wa ngazi za juu muda wowote na mambo yanakaa sawa ambavyo ni tofauti na ilivyokuwa kitambo.
“Ubunge umenipa vitu vingi mno, kwanza kuwatumikia watu wangu kikamilifu kama nilivyokuwa nikihitaji siku nyingi lakini pia napata fursa ya kuonana na watu wazito kama vile waziri mkuu naonana naye muda wowote na kueleza matatizo yaliyopo katika jamii na kupata ufumbuzi au kuyajadili kwa pamoja, kisa kikiwa ni ubunge tu.
“Lakini katika vitu ambavyo sivipendi katika ubunge ni kuitwa mheshimiwa, napenda kuitwa mtumishi. Neno mheshimiwa linatenganisha ukaribu wangu na jamii, wanaweza kuona kama mtu nisiyeguswa badala yake mimi ni mtumishi wao, wanapaswa kuniagiza na kuwatumikia katika mahitaji yao,” alisema Professor Jay.

Leave A Reply