The House of Favourite Newspapers

Tatizo la kulegea kwa misuli ya uke

0

ovariancystdiagram.jpgTatizo hili huwatokea wanawake wengi na huwasumbua sana ambapo katika maisha yao hutokewa na tatizo hili. Ni wachache ambao wanaweza kuliepuka kutokana na sababu mbalimbali za kimaumbile.

Tatizo hili huweza kumuathiri mwanamke kisaikolojia na kimwili kwa ujumla kama tutakavyokuja kuona. Katika hali hii mwanamke hupoteza raha ya tendo la ndoa kutokana na kutokuwepo na msuguano wa kutosha wakati wa tendo.

Kuna mambo mbalimbali yanayosababisha tatizo hili hivyo kufanya liwapate wanawake wote walio katika umri wa kuzaa.

Kwa kawaida uke unatakiwa wakati wote uwe umebana, hii ni kutokana na uimara wa misuli ya chini ya nyonga. Misuli hii ikiwa imara huimarisha mvutiko wake. Misuli hii ya uvungu wa nyonga huweza kukaza daima ili kuwezesha kila kiungo cha kwenye nyonga na chini yake kukaa mahala pake na kuzuia kufanya kazi zisizotakiwa kwa wakati huo. Misuli hii inapopumzika ndipo mtu anapoweza kupata haja ndogo na kubwa.

Wakati wa tendo la ndoa au mwanamke anapozaa pia misuli hii hujiachia kwa kipindi hicho kifupi halafu hukaza tena. Kazi nyingine ya misuli hii ni kuhakikisha viungo vyote vya ndani ya nyonga na kibofu cha mkojo vinakaa mahala pake.

Misuli ya nyonga upande wa chini ndiyo inayowezesha misuli ya uke hivyo huweza kukaza na kulegea kutokana na umri wa mwanamke kusogea au wakati wa ujauzito, kwa hiyo utakuta wengine pamoja na umri kuwa mkubwa lakini misuli yao ya uke inakuwa imara kama bado wasichana, wengine inaachia ili kujiimarisha na kutopata kabisa tatizo hili.

Mazoezi ya viungo kwa ajili ya sehemu hiyo ni muhimu, kuna aina yake ya mazoezi ambayo mwanamke yeyote anatakiwa afanye ili kuepuka asipate tatizo hili la kulegea kwa misuli ya ukeni.

Kulegea huku kwa misuli ya uke kunaweza kuchangiwa na upungufu wa vichocheo mwilini, kukoma hedhi, wakati wa kuzaa anaposukuma mtoto kwa nguvu na kwa muda mrefu, kufunga kupata choo kwa muda mrefu, kikohozi cha muda mrefu na uzito mkubwa. Upo uwezekano wa kurudishia katika hali ya awali misuli ya uke iliyolegea.

CHANZO CHA TATIZO

Kulegea kwa misuli ya uke kunatokana na kulegea kwa misuli ya chini ya nyonga ambayo pia sehemu iliyopo inaitwa ‘Perineum’. Hapa kuna kundi la misuli na nyuzinyuzi zake zinazoshikilia misuli mikuu.

Misuli hii hupatikana kwa mwanaume na mwanamke. Kazi nyingine ya misuli hii ni kusaidia kubeba na kuzuia viungo vyote vya ndani ya nyonga kukaa kwa uimara.

Viungo vya ndani ya nyonga vinavyosaidiwa na misuli hii ni kizazi, mfuko wa haja kubwa na matumbo. Misuli hii huvutika kama mpira na inatakiwa iwe katika hali ya kuvutika muda wote siyo kupwaya.

ATHARI ZA KULEGEA KWA MISULI YA UKE

Athari hutokana na misuli hiyo kushindwa kufanya kazi yake yaani kupwaya na huambatana na matatizo mbalimbali kama mkojo kutoka wenyewe na kushindwa kujizuia, kila wakati kujihisi kupata haja kubwa na ukienda haja inatoka kidogo kidogo, kuhisi kizazi kinashuka, ukikojoa mkojo hauishi, choo kikubwa hata ujikamue vipi hakiishi.

Pia maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa muda mrefu na maumivu ya kiuno, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa na kupoteza hamu na raha ya tendo la ndoa. Wakati mwingine kizazi kinaweza kutoka nje ukeni hasa kwa wanawake wazee.

Pia endapo misuli ya uke itakaza sana mwanamke atalalamika maumivu ya nyonga ya muda mrefu kiasi kwamba anaweza kutibiwa kama tatizo la mifupa lakini bado inaendelea hivyo hivyo, kumbe hapa tatizo kubwa ni kubana zaidi kwa misuli ya ukeni.

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply