The House of Favourite Newspapers

Fahamu Jinsi ya Kupata Mtoto wa Kiume / Kike

0

BAADA ya kuandika makala yangu kuhusu madhara anayoweza kupata mtu kwa kutofanya tendo la ndoa, nimepokea maswali mengi huku wengi  wao wakitaka kujua zaidi kuhusu masuala ya uzazi ikiwemo mambo yanayosababisha kupata mtoto wa kiume ama wa kike.

Kulingana na tamaduni zetu, wengi huwa tunamtanguliza Mungu na kumuomba atupatie mtoto tunayemtaka.

Zipo njia nyingi za kitaalam, ikiwemo ya kupandikiza kizazi Intra Vitro Fertilization (IVF) ama kutumia kalenda.

Mwanamke huzalisha mbegu aina moja ‘XX’ (X-Chromosomes) Mwaanaume anazalishwa mbegu za aina mbili ‘X’ (kike) na ‘Y’ (kiume) (XY-Chromosomes).

Wakati wa uchavushaji; 

Mama akitoa X na baba X = XX (mtoto wa kike)

Mama akitoa X na baba Y = XY (mtoto wa kiume)

Mbegu ‘X’ ni imara ukilinganisha na ‘Y’, pia ‘X’ zinatembea polepole kulinganisha na mbegu ‘Y’ ambazo zenyewe ni dhaifu (sio imara na hufa mapema), lakini zina mwendokasi mkubwa.

 

 

Kalenda

Lazima ujue mzunguko wa mwanamke husika ni wa aina gani… kwa maana kuna mizunguko ya wastani wa siku 28 ambayo hii yai lake hutoka siku ya 14, kuna mzunguko mfupi wa siku 21 na yai hutoka siku ya 10 na pia wale wa mzunguko mrefu wa siku 36 ambao yai hutoka katika siku ya 18.

Mfano unaweza pata HEDHI kuanzia tarehe 1-5 na wengine huchukua siku 7. Hiki ni kipindi ambacho uterus hutoa damu baada ya yai la mwanamke kukosa kurutubishwa na mbegu za kiume.

SALAMA, SIKU YA 6-10. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kupata mimba japo kinaelekea kipindi cha hatari

HATARI, SIKU YA 11-18. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke akijamiiana anapata mimba.

Kama mfumo wake wa uzazi upo sawa. Yaani hana uvimbe sehemu yoyote, homoni zimebalance vizuri, mirija haijaziba, hana infections zozote km vile PID, fangasi na UTI, kizazi hakina mikwaruzo. Hapa atapata mimba bila shida.

SALAMA SIKU YA 19-28. Hiki ni kipindi kingine baada ya Ovulation ambapo mwanamke hawezi kushika mimba. Anajiandaa kupata hedhi nyingine kwakuwa yai halikurutubishwa siku za hatari. Endapo limerutubishwa hawezi ona hedhi nyingine.

Wahusika wakishiriki tendo la ndoa angalau siku ya ovulation (day 14) ama siku mbili au siku ya ovulation (siku yai la mama kukomaa), hapa kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kiume kwa vile mbegu Y husafiri kwa kasi, ndiyo itakayotangulia na hivyo kukutwa na mbegu ya mama wakati nyingine ya X ikiwa imeachwa kwa vile kasi yake ni ndogo.

Wazazi wanaoota kupata mtoto wa wa kike washiriki tendo la ndoa wakati zikiwa zimebaki siku tatu au nne kabla ya yai la mama kutoka, maana yake mwendo wa X utakuwa wa taratibu na itadumu kwa siku hizo nyingi kabla ya kukutwa na kukutana na mbegu itokayo kwa mama wakati mbegu Y ikiwa tayari imeshaharibika kutokana na kutangulia kwake mbele haraka na kukosa uimara wa kusubiria siku zote hizo.

Sperm Motility

Kiwango cha mbegu unachotoa (kwa wanaume). Kama unatoa mbegu nyingi basi una nafasi kubwa ya kupata mtoto wa kiume.

Kutokana na wingi wa sperm, ‘Y’ zina spidi hata kama zitakuwa dhaifu lakini kutokana na wingi wake, baadhi zitakuwa na nyingine zita-survive na kufika kwenye yai la mama na kurutubisha then X ya mama na Y ya baba zitatengeneza XY = mtoto wa kiume.

Alkaline/Acidic

‘Y’ chromosomes zina survive vizuri kwenye njia ya uzazi ya mama yenye ute mchachu (alkaline) na kuharibu ‘X’ chromosomes, ‘Y’ ya baba itapita na kukutana na ‘X’ ya mama kisha kutungisha maana yake atazaliwa kwa mtoto wa kiume.

X chromosomes zina survive vizuri kwenye njia ya uzazi ya mama kali (acidic) na kuharibu ‘Y’ chromosomes, kama X ya baba itapita na kukutana na X ya mama kisha kutungisha maana yake atazaliwa kwa mtoto wa kike.

Umri

Tafiti zinaonyesha kuwa vijana wana sperm motility kubwa hivyo tukirejea kwenye pointi ya sperm motility hapo juu wakati wa kujamiiana, vijana wana possibility kubwa ya kupata mtoto wa kiume. Binti mwenye umri wa miaka 24-35 anazo alkaline fluids nyingi zinazo favor ‘Y’ na kutungisha baby boy.

Sperm motility ya watu wenye umri mkubwa (wazee kuanzia miaka 55 na kuendelea ni ndogo, hivyo wana possibility kubwa ya kupata mtoto wa kike.

 

 

MAMBO YA KUZINGATIA

Ongeza idadi ya mbegu

Mwanaume unatakiwa uongeze wingi wa mbegu zako (sperm count) aidha kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati ukisubiri mke aanze kuona yai linashuka (ovulation day).

Nguo za kubana

Kwa kawaida korodani zinatengeneza mbegu nyingi zaidi wakati wa hali ya ubaridi kuliko kwenye joto hivyo mwanaume unatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, acha kuweka laptop kwenye mapaja, acha kuvuta sigara na kunywa pombe.

Staili za tendo la ndoa

Unahitaji utumie staili ambazo zinawezesha mwingiliano mkubwa (deep penetration) na hii ni mhimu hasa kama wewe mwanaume una umbile dogo.

Staili hizi huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume yaani XY kufika haraka na kufanya utungwaji wa mimba kuwa rahisi.

Wakati unapotumia staili za mwingiliano mdogo (shallow penetration) husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa wa uzazi, hivyo mbegu hukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike (XX) kutungisha ujauzito na hapo anatokea mtoto wa kike.

Kufika kileleni

Mwanaume hakikisha mkeo anafika kileleni kwanza kabla ya wewe. Mwanamke anapofika kileleni huwa anatoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo huwa haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.

Sasa mwanaume utahitaji kuchelewa kufika kileleni lakini uonapo tu mama amefika kileleni basi na wewe ufike muda huo kabla hakujakauka namna rahisi kama wewe ni mtu wa kufika kileleni haraka ni kumuandaa vya kutosha mkeo.

Vyakula

Mwanamke anatakiwa kwa kipindi kirefu ale vyakula na anywe vinywaji visivyo na asidi (tindikali) vitu vinavyoongeza asidi mwilini ni pamoja na vyakula vya kusisimua (spiced foods), vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, pombe, chai ya rangi, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, maziwa na bidhaa zingine zitokakanazo na maziwa n.k.

Vyakula visivyo na asidi nyingi ni pamoja na matunda, mboga za majani, maji ya kunywa, mbegu mbegu (za karanga, za ufuta, korosho, za maboga nk), apendelee kula uyoga pia.

 

Leave A Reply