The House of Favourite Newspapers

Ngozi yako imekufa? Maziwa ya unga yatakusaidia

0
concept of cosmetic effects, treatment and skin care. face of young woman with dry skin
concept of cosmetic effects, treatment and skin care. face of young woman with dry skin

Watu wengi sasa hivi wameharibika nyuso zao kutokana na hali ya upepo ambao unasababisha ngozi kuwa mbaya na wengi wamejikuta kila mara wakibadilisha mafuta au cream ya kupaka bila mafanikio.

Leo nikupe ujanja shosti, nataka kukusaidia jinsi ya kuifanya ngozi yako iwe nyororo kwa kutumia scrub ya maziwa, asali na limao.

Mahitaji

Chukua maziwa ya unga, asali, juisi ya limao na mafuta ya mzaituni au mrozi

 Baada ya hapo…

Changanya kila kitu kwa usawa, kama ni kijiko kimoja cha asali, juisi ya limao na mafuta ya mzaituni au mrozi vyote viwe sawa. Kama umeamua kutumia nusu kikombe pia unaweza kuvilinganisha vyote.

Baada ya kupata mchanganyiko huo changanya na maziwa ya unga kisha ukoroge mpaka upate mchanganyiko mmoja. Ukishakuwa unavutika kama cream, paka kwenye ngozi yako.

Kaa kwa muda wa dakika 15 kisha fanyia masaji taratibu. Baada ya hapo osha kuondoa scrub yote. Maziwa yanaifanya ngozi yako kuteleza na kuwa nyororo. Pia inapambana na madhara ya jua na kukufanya uonekane mrembo zaidi.

Asali inaifanya ngozi yako kung’aa zaidi kwani ina kitu kinachong’arisha, limao linakusaidia ‘kubreach’ ngozi na kuifanya kuwa ya asili zaidi.

Mafuta ya mzaituni au mrozi yanaifanya ngozi iliyokufa iondoke na kupata ngozi nzuri.

Leave A Reply