The House of Favourite Newspapers

R.O.M.A afunguka ‘kumkopi’ Eminem

0

ROMAMKATOLIKI3Ibrahimu Mussa ‘R.O.M.A’

Makala: Erick Evarist

WASANII wengi Bongo kabla ya kuanza sanaa walikuwa na watu wanaowavutia kufanya muziki. Ibrahimu Mussa ‘R.O.M.A’ naye aliguswa sana na msanii kutoka Marekani, Marshall Bruce Mathers III ‘Eminem’.

Katika makala haya, R.O.M.A anamfungukia msanii huyo hususan baada ya BMM (Burudani Mwanzo Mwisho) kumbana kwa kuona katika wimbo wake mpya uitwao Kaa Tayari aliouachia wiki iliyopita, mkali huyo amechana kama Eminem.

1372520844_eminemg.jpgMarshall Bruce Mathers III ‘Eminem’.

BMM: ‘Idea’ (wazo) ya Kaa Tayari ilikujaje kwenye ubongo wako?

R.O.M.A: Kaa Tayari ni chakula kipya au chakula kigeni katika matumbo ya mashabiki wa R.O.M.A, kwenye Muziki wa Hip Hop! Ni R.O.M.A ambaye pengine wengi hawajamzoea katika staili, mpangilio na muundo wa video zake… kwa hiyo unapowapa watu chakula kipya ambacho hawajakizoea kwenye midomo na matumbo yao, inabidi uwaandae kwa kuwaambia kaeni tayari.

BMM: Sasa umewaambia mashabiki wakae tayari, ina maana kuna mabadiliko yanakuja au ndiyo tayari yapo kwenye hiyo ngoma?

R.O.M.A: ‘Of course yes!’ Ngoma yenyewe inaitwa Kaa Tayari! Na ukiisikiliza utaona mabadiliko yenyewe! Ya staili, mtiririko, mdundo hadi muonekano wa video, kitu ambacho R.O.M.A hakukifanya kabla.

BMM: Video umefanya na nani na ni mabadiliko gani uliyoyafanya?

R.O.M.A: Video amefanya dairekta Nick Dizzo kutoka Kampuni ya Focus Film! Muonekano wa video ni tofauti na video zangu zilizopita! ‘Quality’ ya picha, watu wanaoonekana kwenye video na ‘video queens’ ni sura ngeni kabisa! Tumewaweka kuongeza ladha tofauti itakayomvutia mtazamaji wa rika lolote na jinsia yoyote!

BMM: Kwa nini ulifikiria kuwashirikisha Darasa na Jose Mtambo na si wasanii wengine?

R.O.M.A: Darasa ni shule na R.O.M.A ukiisoma kwa kuunganisha ni kanisa, Jose ni mtambo! Kwa hiyo inakuwa ni shule, kanisa na mtambo wa kukaa tayari!

BMM: Kwa nini ngoma zako nyingi unafanyia Tongwe Records?

R.O.M.A: Mara nyingi natazama uzuri wa kazi haijalishi itakuwa ni katika studio hiyohiyo au la! Kama kazi ni nzuri basi ifanyike tu hata kama ni hapohapo! Tongwe ni nyumbani kabisa kwa hiyo nakuwa huru zaidi kufanya kazi nyumbani japo nimeshafanya kazi na maprodyuza wengine kama T-Touch, Dunga, Tuddy Thomas, P-Funk, DX, Issam Touch na Bob Junior.

BMM: Twende kwenye ngoma yenyewe sasa…

R.O.M.A: Twende…

BMM: Wakati ngoma inaanza unasikika kama Eminem, kuna uhusiano wowote kati yako na huyo jamaa?

R.O.M.A: Hahaa! Wengi wanasema hivyo! Sidhani kama nasikika hivyo….labda tu ni kile ‘kidhungu’ nilichoanza nacho (Nowadays, things are changing, I’m going crazy…) Eminem ni ‘role model’ wangu ni miongoni mwa wasanii ninaowapenda sana!

BMM: Tuendelee. Uliposema when I’m gone, mikoba nt’awapa Central Zone ulikuwa na maana gani?

R.O.M.A: Central Zone ni wadogo zangu! Nina msanii wangu anaitwa Monii anatokea kwenye kruu hiyo, ameimba wimbo unaoitwa Kirikuu/Sembe Dona na tupo nao Tongwe tunawasapoti waje kurithi hii mikoba yetu. So ni ile hali ya kutengeneza akina R.O.M.A wengine ili baadaye waendeleze sanaa hii.

BMM: Uliposema gemu inaendeshwa kibepari ulikuwa na maana gani na labda kivipi?

ROMA: Daaah! Gemu yetu ina miungu watu wachache ambao wanaiendesha kimabavu, kibabe na kibepari… muda wowote wakitaka kukuzima wanakuzima, hata kama una kipaji kikubwa jamii inakusahau. Wanakuua!

BMM: Umeshawahi ‘kuuliwa’ na hao mabepari?

Roma: Walijaribu lakini Mungu ananilinda! Napambana!

BMM: Vipi pale uliposema kila demu anaishi Mbezi, ulitaka kufikisha ujumbe gani? Au ndiyo zile za ‘kujaziamo’ vina?

R.O.M.A: Sio kuungaunga vina, kwenye kila ninachotamka kwenye ngoma yangu kina ujumbe, pale nilikuwa namaanisha siku hizi hatuko ‘real’, tunadanganya sana! Mtu hataki kuukubali uhalisia wake na ukweli,hasa mademu.

BMM: Na pale uliposema bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top (hakumtaja jina katika wimbo) ulimaanisha nini?

R.O.M.A: Ewaaaa… apo chacha! Maana’ke ni tusisahau tulipotoka, haijalishi tumefanikiwa kiasi gani ila tusiache asili yetu!

BMM: Unataka kutuambia huyo bosi kaisahau Tip Top?

R.O.M.A: Mitaa inaongea! Na mimi naiwakilisha mitaa.

BMM: Hebu turudi nyuma kidogo, kabla hujamtaja bosi huyo wa Tip Top, ulianza na mstari unaosema: …siku hizi glasi si chochote watu wana red cup… Ulimaanisha nini?

R.O.M.A: Siku hizi glasi sio chochote… watu wana red cup, bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top maana yake; glasi ziko delicate sana ndiyo watu wanazisahau na kukumbatia vile vikombe vyekundu  ambavyo sio delicate kama glasi.

BMM: Uliposema we kimbunga? Nakupiga ka’ Tsunami, ulimaanisha nini?

R.O.M.A: Hiyo ni mistari ya majigambo… We Kimbunga mi nakupa Katrina mixer Tsunami!  Kuwa kama wewe unajiona bora mithili ya kimbunga (upepo) basi mimi ni zaidi ya hiyo… nakupa Katrina na kama haitoshi nakupa Tsunami.

BMM: Kuna taarifa za mitaani zinadai mistari hiyo umemdiss msanii mwenzako, Kimbunga. Kuna ukweli wowote?

R.O.M.A: Nimelisikia hilo kwa watu wengi… jamaa ni mtu wa nyumbani kwetu, sijamdiss kabisa! Majina tu ndiyo yamegongana.

BMM: Ok, kuna pale sijui…ukitaka vishada nunua simu tanashati (smart phones). Hapo pakoje?

R.O.M.A: Vijana wanakula ngada wanaenda na wakati na ukitaka vishada, nunua simu tanashati! Simu tanashati ni smart phone (simu za kisasa). Ngoma inaanza na neno nowadays (siku hizi)! Kwa hiyo najaribu kuongelea mambo yanayotokea siku hizi.

BMM: R.O.M.A nakushukuru.

ROMA: Barida!

Leave A Reply