The House of Favourite Newspapers

Gwiji wa Filamu Anayesujudiwa India

0

kabali-1

Rajinikanth.

WATU wengi walio nje ya nchi ya India hawamjui Rajinikanth, mwanamme shupavu mwenye umri wa miaka 65, ambaye pia ni muigizaji shujaa, anayependwa na zaidi ya watu milioni kumi duniani kote na anayeabudiwa kama muungu.

Rajinikanth, alianza kufahamika katika ulimwengu wa filamu miaka arobaini iliyopita. Tayari amecheza filamu nyingi na flamu yake ya mwisho ameitoa mwezi Julai 22, 2016. inayoitwa Kabali.

Marekani peke yake filamu ya Kabali tayari imeingiza pesa taslimu inayokadiriwa kufika dola za Marekani $4.1 kwa kuuza tiketi pekee za uzinduzi wa filamu hiyo na kushika nafasi ya tisa ya filamu bora za mwezi Julai ikiwa ni filamu pekee iliyoigizwa kwa lugha isiyo ya kiingereza kwenye filamu kumi bora.

Nchini India pekee, tayari filamu ya Kabali imeingiza zaidi ya dola za Marekani milioni 16 na kuwapita mastaa wa Bollywood, Sultan na Salman Khan.

kabli-story-6147_061616080338

Kufanikiwa kwa Rajinikanth, katika masuala ya kiuchumi kumechangiwa sana kuwa na kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa vyoo na chocolate.

Wakati wa uzinduzi wa filamu ya Kabali makampuni mengi makubwa nchini India kwenye majiji ya Bangalore na Chennai yalitangaza siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wake ili wapate muda wa kutazama uzinduzi wa filamu hiyo mpya.

Mfanyabiashara Manoj Pushparaj, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Waterproofing, iliyopo jijini Bangalore, aliwapa mapumziko wafanyakazi 40 wapate kuhudhuria uzinduzi huo akiamini kwamba kazi hazitofanyika kwenye kiwango kilicho bora.

Uzinduzi huo umelinganishwa na mechi maarufu ya kriketi kati ya timu yao ya taifa na ile ya Pakistan ambao kihistoria ni watani wa jadi wa mchezo wa kriketi siku wanapokutana japo wafanyakazi huenda kazini lakini akili zao na mawazo yao huwa kwenye kufuatilia mchezo huo.

160726144658-air-asia-exlarge-169

Kampuni kubwa ya ndege ya AirAsia wao waliunga mkono uzinduzi huo kwa kuweka bango la picha ya Rajinikanth kwenye ndege yao inayofanya safari kati ya Jiji la Bangalore na Chennai kama ishara ya kumuunga mkono.

Leave A Reply