The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba na Katibu wa Mkoa Watumbuliwa

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi Said - RTX1TYDQ

Rais John Magufuli.

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Taarifa hiyo  iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Kadhalika Rais Magufuli leo amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545milioni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016.

Comments are closed.