Winga Ajirekodi Akifanya Ngono, Awatumia Video Mashabiki

AIBU kubwa imemkuta winga wa zamani wa Tottenham, Mcameroon, Clinton N’Jie ambaye hivi karibuni alijikuta akitazamwa na mamilioni akifanya ngono, baada ya kutuma video yake kimakosa mtandaoni akiwa bize akifanya kitendo hicho.

 

N’Jie, 25, alikuwa akifanya ngono lakini ghafla akabonyeza kitufe tofauti ambacho kilisababisha arushe mubashara tukio lake hilo kwenye mtandao wa SnapChat na kuonwa na mamilioni ya wafuasi wake kabla hajaifuta video hiyo.

 

Hata hivyo, baada ya kufuta video hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshatazamwa, N’Jie aliomba radhi akisema alikuwa amelewa sana kutokana na furaha aliyokuwa nayo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na Klabu ya Dynamo Moscow ya Urusi akitokea Olympique Marseille ya Ufaransa.

 

Baada ya kusaini mkataba huo, inadaiwa kuwa N’Jie alitaka kuingia kwenye Google ili aisome habari yake lakini akajikuta akibonyeza kitufe kingine kimamosa kilichosababisha arushe ‘live’ tukio lake akifanya ngono na mwanamke mmoja aliyekuwa amesuka nywele.

 

“Samahanini, nililewa sana. Nilisherehekea mkataba wangu mpya. Nilibonyeza kitufe tofauti,” alisema kwa aibu. N’Jie alifunga mabao matatu katika mechi 17 za Ligue 1 msimu uliopita.


Loading...

Toa comment