The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Upelelezi Aliyehukumiwa Kunyongwa Akwama Kortini

MAHAKAMA ya Rufani imetupilia mbali maombi ya marejeo ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

 

Mwaka 2016, Bageni aliwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo akiiomba mahakama hiyo ibadilishe uamuzi wake.

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Azam TV, uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi hayo, umetolewa leo, Jumatano, Agosti 14, 2019,  na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu.

Comments are closed.