The House of Favourite Newspapers

A-Z Arusha Watoa Mashuka 100 Kwa Serikali

0

Kiwanda cha A-Z kilichopo mkoani Arusha leo Aprili 22, 2020 kimekabidhi jozi ya mashuka mia moja kwa Serikali mkoani Arusha kuwasaidia wagonjwa watakaokuwa karantini kuunga mkono Serikali dhidi ya mapambano ya Virusi vya Corona nchini.

Msaada huo umepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega na ametoa shukrani kwa niaba ya Serikali na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Pia amewataka wananchi kuendelee kuchukua Tahadhari zote za kiafya ili kujikinga na Corona kama inavyoshauriwa na wataalamu Wa Afya.

Leave A Reply