The House of Favourite Newspapers

ABB Yashinda Maombi ya Mfumo wa Kuwianisha Umeme kutoka Hitachi

KAMPUNI ya ABB leo imetangaza kwamba Hitachi, Ltd. (TSE: 6501, “Hitachi”) imetoa maombi ya kupatiwa mfumo wa ABB Ability™ Network Manager Market Management System (MMS), ambayo ni program kwa ajili ya kuweka uwiano sawa katika mfumo wa soko la umeme.

 

MMS, ambao ni mfumo wa usimamizi wa masoko, ukiwa na njia mbalimbali za matumizi ya kisasa yanayotoa nguvu katika majukumu mbalimbali ya masoko na miundombinu ya teknolojia ya habari (IT), itatumika kulingana na mahitaji ambayo ni maalum katika kuweka uwiano katika masoko ya umeme ambapo kampuni ya TEPCO Power Grid, Inc. na Chubu Electric Power Co. yanauendeleza kwa niaba ya kampuni iliyoenea nchini kote ya Transmission System Operators (TSOs).

MMS itakuwa kama jukwaa litakalowezesha mawasiliano ya uwiano katika masoko ya umeme ambayo yataanzishwa Aprili 2021. Kuna mabadiliko yanayoendelea katika mfumo wa umeme nchini Japan na ufumbuzi huu wa kidijitali utatumika katika vyombo husika kuwezesha uwiano katika manunuzi thabiti katika uwezo na nishati husika. Pamoja na kuimarisha utendaji wa masoko, mfumo huu utachangia katika utoaji wa umeme wa kuaminika.

 

“Hitachi na ABB kwa kupitia matumizi ya ABB Ability™ Network Manager MMS, huwezesha utendaji kazi mathubuti na wenye kuaminika katika kuweka uwiano wa masoko ya umeme,” alisema Massimo Danieli, mkuu wa shughuli za mfumo wa kujiendesha wenyewe katika njia kuu za kumeme za kampuni hiyo.

 

Anaongeza: “Ushirikiano mkubwa kati ya makampuni haya mawili utaimarisha mfumo wa umeme nchini Japan na matumizi ya dijitali katika kujenga mfumo imara na mzuri zaidi wa kusafirisha na kugawa umeme.”

 

Mfumo wa MMS kwa ABB umekubalika kama ufumbuzi mpya wenye ubunifu katika kuweka uwiano sawa barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini. Ni ufumbuzi uliothibitika ambao unahakikisha utendaji kazi thabiti na endelevu wa mfumo husika ambao wakati huohuo unaendeleza uimara katika masuala ya ugavi wa umeme.

 

Hitachi na ABB zilifikia makubaliano ya ushirikiano mnamo Desemba 2017 na zilianza kushirikiana katika program mbalimbali ikiwemo ya MMS. Katika kujiimarisha kutokana na ushirikiano huu, Hitachi na ABB zimedhamiria kuyakabili mahitaji ya matumizi ya kidijitali katika mfumo wa umeme nchini Japan.

 

Katika ushirikiano huu, makampuni hayo mawili hujumuisha nguvu zao katika kuunga mkono makampuni mbalimbali ya zana na yenye kuzalisha nishati nchini Japan. Ni muungano wa teknolojia ya Hitachi na utaalam ambao umelimbikizwa kwa kutoa vifaa na mifumo mbalimbali ya umeme nchini Japan na teknolojia iliyothibitishwa ya program ya ABB.

ENDS

ABB (ABBN: SIX Swiss Ex) ni wataalam wakubwa wa huduma katika viwanda vinavyotumia mfumo wa dijitali. Ikiwa na historia ya uvumbuzi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 130, ABB leo hii inaongoza katika masuala ya viwanda vya kidijitali katika miradi mikubwa minne yenye kulenga kutoa huduma kwa wateja mbalimbali duniani ambayo ni: Uenezaji wa Umeme, Mashine Mbalimbali, Robot na Zenye Kujiendesha Zenyewe, zikiimarishwa na jukwaa la dijitali la ABB Ability™. Shughuli za Mitambo ya Umeme ya ABB zitapelekwa kwa Hitachi mwaka 2020. ABB inafanya kazi katika nchi zaidi ya 100 ikiwa na wafanyakazi wapatao 147,000.

Comments are closed.