The House of Favourite Newspapers

Abood Apita Bila Kupingwa Morogoro Mjini

0

Msimamizi wa Uchaguzi Morogoro Mjini, Sheila Lukuba amempitisha Abdulazizi Abood (CCM) kuwa mgombea pekee wa Ubunge Jimbo hilo baada ya wagombea wengine kukatwa kwa kile alichotaja ni kutokana na makosa yaliyobainika katika ujazaji fomu.

 

Msimamizi wa Uchaguzi huo,  amewafutilia mbali wagombea wote wa vyama vya upinzani akiwemo Devotha Minja wa CHADEMA na kumbakiza Abdulaziz Abood wa CCM kuwa mgombea pekee, kwa madai kuwa wagombea wa upinzani walikosea kujaza fomu.

Tayari Msimamizi huyo amemtangaza Abood kupita bila kupingwa. Hii ina maana kuwa hatafanya kampeni wala kupigiwa kura bali atasubiri kuapishwa tu. Wagombea waliokatwa ni wa CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF na CHAUMA. Hata hivyo CHADEMA wamesema watakata rufaa kupinga maamuzi hayo.

Leave A Reply