The House of Favourite Newspapers

UVCCM: Asante kwa Kazi Kubwa Rais Samia, Piga Kazi Mama

0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa Kenan Kihongosi

Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM limeaziamia kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea Watanzania Maendeleo

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa dhamira na nia moja umempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku ya shilingi Bilioni 100 ili kupunguza ukali wa bei ya Mafuta na kuanzia jana tumeona bei zimeshuka

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza Kuu UVCCM Taifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa Kenan Kihongosi amesema

“Tunampongeza Mhe. Rais kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa 1500 nchi nzima hii ni hatua kubwa kwani imepunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa madarasa na wananchi wanafuruhia hili kwani watoto wao wote waliofikisha umri wa kwenda shule wanaenda bila vikwazo”

“Tunampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya Uzinduzi wa Royal Tour na kuitangaza nchi yetu na tumeona watu maarufu ulimwenguni na Watalii wengine wengi wameanza kumiminika nchini haya yote ni matokeo ya Filamu ya Royal Tour”

Aidha Ndugu Kihongosi amesema Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hasaan imenunua Ambulance takribani 390 na ujenzi wa Hospitali na vituo vya Afya lengo likiwa ni kuboresha Afya za Watanzania.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu UVCCM Taifa amesema “Mhe Rais Samia Suhuhu Hassan ametoa fedha takribani milioni 10 kila Mkoa ili kuboresha Ofisi za Machinga na kuwajengea muunganiko katika shughuli zao na katika hili muhimu apongezwe kwa kugusa Maisha ya kundi hili muhimu katika nchi yetu.

Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa; “Tunapenda kumtia Moyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na tunampongeza kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea Watanzania maendeleo, tunamuahidi tutamlinda na kuendelea kuyasemea mema mengi anayoyafanya katika nchi yetu,” amesisitiza Kihongosi.

Leave A Reply