The House of Favourite Newspapers

Rais Museveni akutana na Balozi wa Urusi

0

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jana Machi 3, 2022 alikutana na balozi wa Urusi, Vladlen Semivolos kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na mkutano huo, lakini hii inakuja siku moja baada ya Uganda kutopiga kura kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Nchi nyingine 16 za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Angola, Algeria na Mali hazikupiga kura.
Mtoto wa kiume wa Rais Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jumatatu alieleza kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika ujumbe wa Twitter.

Leave A Reply