The House of Favourite Newspapers

Acacia Waamua Kupunguza Operesheni Mgodi wa Bulyanhulu

0

KAMPUNI ya Acacia imetangaza lengo lake la kupunguza shughuli za uendeshaji na uzalishaji katika Mgodi wa Bulyanhulu kutokana na upungufu wa mzunguko wa pesa uliosababishwa na zuio la usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi na mazingira ya uendeshaji kuwa magumu.

Tangu zuio la mchanga wa dhahabu na shaba liwekwe na Serikali mnamo Machi 3, 2017 na kuathiri takribani 35% ya uzalishaji wa mwaka, Acacia imekuwa na takribani mchanga wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 265 ndani ya nchi kulingana na bei za sasa

Katika kusaidia kukabili hasara hizi, Acacia imeamua kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupunguza uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu ili kulinda ajira za wafanyakazi na watoa huduma mgodini ambao ni Watanzania.

Kampuni ya Acacia bado ina matumaini katika majadiliano yanayoendelea kati ya Barrick na serikali ikiamini yatapelekea muafaka juu ya zuio la makinikia na mazingira ya uendeshaji yatakayowezesha tathmini mpya ya hali ya uendeshaji kwa siku zijazo.

 

Wakazi 2000 Mara Wakosa Maji Baada ya Mwenzao Mmoja Kuyazuia

Leave A Reply