The House of Favourite Newspapers

Achana na Muziki, Darassa Sasa; ni Zamu ya Mademu, Unga na Mitungi Kwenda Mbele

darasaStori na Hashim Aziz | Gazeti la Uwazi, Toleo la Jumanne, Jan 10, 207

“WAKIOTA mapembe waongezee mkia, na ukinibeep tu nakupigia…sio simba sio chui sio mamba aaahhh!  Ngozi yangu inatosha kujigamba…” hayo ni mashairi yanayobamba kinomanoma kitaa, ya mkali Shariff Thabeet wakuitwa Darassa! Ngoma inaitwa Muziki, ukiita wimbo wa taifa utakuwa hukosei.

Yawezekana wengi wamemjua Darassa baada ya kuachia ngoma ya Muziki lakini binafsi namjua mchizi kitambo, tangu enzi hizo anatoka na Sikati Tamaa ambao kama ilivyo kwa Muziki, alimshirikisha Ben Pol. Nilipata nafasi ya kumsikiliza Darassa juzikati katika mahojiano maalum, alipokuja kwenye chumba cha habari (News Room) ndani ya Global Publishers na mwenyewe anakiri kwamba haikuwa rahisi kufika hapa alipofika leo! Anaujua msoto, amepitia maisha ya kigumu, ameishi ‘magetoni’ lakini sasa nyota ya jaha imemuwakia.

Darassa sasa ni supastaa mkubwa Bongo, huwezi kupita sehemu tano kunakopigwa muziki ukakosa kusikia wimbo wake wa Muziki ukipigwa! Nyota yake imeng’ara kiasi cha kuwafunika kabisa wakali kama Diamond Platnumz, Ali Kiba na wengine wengi ambao walikuwa wakishikilia usukani! Kila sehemu sasa hivi utasikia “…acha maneno weka muziki!” Notorious B.I.G enzi za uhai wake, amewahi kuimba, More Money More Problems!

darassaKwa tafsiri nyepesi alimaanisha unavyopata fedha nyingi ndivyo unavyokumbana na matatizo mengi zaidi! Mara nyingi watu tuliozoea kuishi maisha ya chini, ndoto zetu huwa ni kukamata mkwanja! Na tukishakamata mkwanja tu, tunatoka kabisa kwenye tabia zetu halisi na kuingia kwenye maisha ya tofauti kabisa, yanayoongozwa na nguvu ya mkwanja!

Ipo wazi kwamba ukali wa ngoma ya Muziki ya Darassa, hauishii kwa mimi na wewe kuruka kwa furaha, tukiinua mikono juu kwa ile staili ya ‘kigangstar’ kama mwenyewe anavyocheza kwenye video ya wimbo huo, bali mifuko ya mchizi nayo inatuna! Darassa anapiga shoo kila sehemu, leo utasikia yupo huku, kesho kule na kote ‘anasepa na kijiji! Mashabiki kibao wanajaa kwenye shoo zake, anapiga hela ya nguvu! Lakini je, Darassa anautumia vipi mkwanja anaoupata?

Unapokuwa na pesa, utakutana na marafiki na kampani ambazo kama usipokuwa makini, utajikuta ukiishia mahali ambapo hukutarajia. Kila mtu ana hamu ya kukutana na Darassa kwa sasa, kukaa naye, kupiga stori, kula bata na ni wazi kwamba hiki ndicho kipindi ambacho Darassa atapata marafiki wengi kuliko kipindi chochote maishani mwake.

Ndani ya kundi hilo la marafiki, watakuwepo wema lakini wengi watakuwa ni wabaya kwa sababu mara zote marafiki wema ni wale unaokuwa nao unapokuwa kwenye msoto! Wapo watakaomshawishi kwamba kwa sababu tayari ameshakiki kwenye gemu, aweke muziki pembeni na sasa ni muda wa mademu, unga na mitungi kwa sana!

Wapo marafiki watakaothubutu kumkuwadia kwa mastaa wa kike Bongo, wengine wanaweza hata kumpelekea warembo nyumbani kwake au popote alipo ilimradi nao wapate chochote kitu! Wapo watakaomshawishi ajidunge madawa ya kulevya ili apate ‘stimu’ za kistaa na kujiona kama yupo mbele vile!

Wapo watakaokuwa wakimpa mialiko ya kula gambe usiku kucha! Si pesa ipo! Si jina limekuwa kubwa! Wapo watakaomshawishi hata kuwekeza pesa anazopata kwenye biashara haramu ya madawa ya kulevya! Ndiyo! Pesa mwanaharamu. Ninavyomjua Darassa ni mwana fulani ambaye kichwani yupo poa!

Ana akili na ndiyo maana hakukata tamaa kipindi chote hicho mpaka leo ametoboa lakini ushawishi wa watu wanaomzunguka ndiyo unaonipa mashaka. Atakapoteleza kidogo na kuwapa nafasi marafiki ndiyo wamchagulie aina ya maisha ya kuishi, ataweka muziki pembeni, itakuwa ni yeye na mademu, mademu na yeye!

Itakuwa ni yeye na ‘ngada’, ‘ngada’ na yeye! Itakuwa ni mitungi kwa kwenda mbele na kama shetani huyo akimganda, basi Muziki ndiyo itakuwa ngoma yake ya kwanza na ya mwisho kubamba! Mengine yatabaki kuwa historia inayojirudia, kama ilivyotokea kwa marehemu Albert Mangweha (Ngwair), Langa, Chid Benz na wengine wengi ambao nguvu ya ustaa iliwazidi na kujikuta wakiishia kupotea kwenye gemu, wengine wakipoteza kabisa maisha na wengine wakiishia kuwa ‘mateja’ wa kutupwa! Akili kumkichwa Darassa!

Umehangaika sana kufika hapo ulipo, na ndiyo kwanza umeanza kula matunda ya jasho lako! Waepuke marafiki wabaya, epuka mtindo mbovu wa maisha, kuwa makini na mkwanja unaoingiza kwa sababu huijui kesho yako… ukizingatia ushauri wangu, utaendelea kutengeneza mkwanja kama alivyofanya Diamond Platnumz. Ukipuuza, ukataka kukimbia wakati hauna breki, basi utavuna ulichokipanda! Watch yourself usije ukajiconfuse! Vitu vingine havitakagi ujuaji!

Comments are closed.