The House of Favourite Newspapers

Aeshi Hilaly: Itafika Mahali Tutashikana Mashati Humu Bungeni – VIDEO

Mbunge wa Sumbawanga Mjini kupitia tiketi ya CCM, Aeshi Hilaly amesema kwamba kitendo cha serikali kuzuia wakulima wa mahindi kuuza nje ya mipaka ya nchi, ni kuwaumiza mno wakulima wanyonge, ambao wanahangaika kwa kipindi kirefu kuzalisha mazao yao kisha wanapangiwa sehemu ya kwenda kuuza.

 

Mbunge huyo amesema kwamba itafika mahali, wabunge watachoka kuzungumza na kushikana mashati bungeni kwa sababu kila sekta, wananchi wanaowawakilisha wananyanyasika, kuanzia kwa wakulima mpaka wavuvi.

 

VIDEO: Msikie Akifunguka

Comments are closed.