The House of Favourite Newspapers
gunners X

AFCON: Diarra Aang’ara, Mali Yaipiga Tunisia kwa Matuta 3–2 Yatinga Robo Fainali

0

Kipa Djigui Diarra na wenzake wa Timu ya Taifa ya Mali wametinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 3–2 dhidi ya Tunisia, kwenye Uwanja wa Mohammed V, Casablanca hatua ya 16 bora.

Mchezo ulimalizika kwa sare ya 1–1 ndani ya dakika 120. Tunisia walitangulia kupata bao kupitia Chaouat dakika ya 88, kabla ya Sinayoko kuisawazishia Mali dakika ya 90+6.

Katika mikwaju ya penalti, Mali walionesha utulivu na kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.

Matokeo ya Mwisho
Mali 1–1 Tunisia
(Penalti: Mali 3–2 Tunisia)

Waandishi wa mabao

  • Mali: Sinayoko 90+6’

  • Tunisia: Chaouat 88’

Mikwaju ya penalti

  • Mali: ❌ ✅ ❌ ✅ ✅

  • Tunisia: ✅ ❌ ✅ ❌ ❌

Kwa matokeo haya, Mali sasa watakutana na Senegal katika hatua ya robo fainali.

Leave A Reply