The House of Favourite Newspapers

Afisa Mkuu wa Usalama wa Zamani wa Twitter Afichua Mapungufu ya kiusalama kwa watumiaji Wake

0
Twitter ni mtandao usiokuwa na usalama wa faragha kwa mujibu wa Zatko

MKUU wa usalama wa Twitter aliyefutwa kazi hivi karibuni anadai kuwa mtandao huo wa kijamii unatishia ufaragha kwa watumiaji wake milioni 238 kila siku, yakiwemo mashirika ya serikali na maafisa, jambo linalohusisha usalama wa Taifa.

 

Madai hayo yalitolewa na Peiter Mudge Zatko, mdukuzi huyo wa kompyuta ambaye alikuwa ameajiriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Twitter Jack Dorsey.

 

Shutuma za Zatko, ikiwa ni pamoja na madai ya “upungufu mkubwa na mbaya” katika mazoea ya Twitter ya kukabiliana na barua taka na udukuzi, zimo katika hati ya mtoa taarifa iliyotumwa Julai 6 kwa mashirika matatu ya serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Idara ya Haki.

Peiter Mudge Zatko

CNN na The Washington Post ziliripoti maelezo ya malalamiko hayo siku ya Jumanne, Toleo lililorekebishwa la hati hiyo ya kurasa 84 lilitumwa kwa Bunge la Marekani.

 

Zatko “alifutwa kazi katika wadhifa wake mkuu katika Twitter mnamo Januari 2022 kwa uongozi usio na tija na utendakazi mbaya,” msemaji wa Twitter, ambaye hakutaka kutambuliwa kwa jina, alisema katika taarifa kwa VOA.

 

Imeandikwa: Leokadia Charles kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply