The House of Favourite Newspapers

Ofisa TRA Adakwa na PCCB Kwa Kuomba Rushwa Mil. 50

OFISA Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38), anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh milioni 50 na kupokea Dola za Marekani 1,000 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa Agosti 2, 2019  Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo,  amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba rushwa kwa mfanyabiashara raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HEM Heavy Equipment Company Ltd.

 

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara huyo kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

 

“Kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000 ili aweze kumsaidia mfanyabiashara huyo.

 

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000),” alisema.

ONA MISS LAKE ZONE 2019 ALIVYOTANGAZWA FULL SHANGWE!

Comments are closed.