The House of Favourite Newspapers

Agoma Kula kwa Siku 141

0

MWANAUME mmoja wa Kipalestina aliyetambulika kwa jina la Hisham Abu Hawash (40) amegoma kula na kushinda njaa kwa siku 141 akishinikiza kuachiliwa baada ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Israel kumshikilia tangu Februari mwaka jana bila ya kumfungulia mashtaka.

Hisham ambae ni baba wa watoto watano, Inadaiwa kuwa ni mfuasi wa kundi la wanamgambo wa kundi la Islamic Jihad. Alianza mgomo akishinikiza kupinga mfumo wa Israel wa kuwaweka watu “vizuizini”, ambapo watu wanaweza kushikiliwa kwa miaka mingi bila kufunguliwa mashtaka ama kuwa na vielelezo vya ushahidi dhidi yao.

Mwanasheria wa Hisham, Jawad Boulos amesema mteja wake alikubali kusitisha mgomo wa kula baada ya Israel kuahidi kumwachilia huru mnamo Februari 26.

Leave A Reply