The House of Favourite Newspapers

Ahmed Ally Afungukua Kuelekea Derby -”Tutampelekea Pumzi Ya Moto, Azam Washamaliza Mwendo”- Video

0

MENEJA wa Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo.

“Mchezo dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya Jumapili Novemba 5, 2023 saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa. Ni mechi kubwa kwetu, ni mechi ambayo inakwenda kuonyesha ubora halisi ya mpira wa Tanzania na ushindi wake unaleta tabasamu kwa mashabiki wa timu husika na kupoteza kunaacha majonzi.”

“Ni mechi ambayo Wanasimba inabidi tujitoe muhanga ili kupata ushindi. Kila Mwanasimba ajue ana jukumu la kusaidia timu yake. Tukishinda siku hiyo shughuli itakuwa imeisha, itabaki shughuli ya kukamilisha ratiba ya msimu.”

“Raha ya msiba waliaji wawe wengi, tunawaomba mashabiki wao waje uwanjani na wakae hadi mwishoni sio tukishawafunga wawahi kuondoka, wasubiri hadi mchezo uishe.”

“Viingilio Mzunguko – Tsh. 5,000, Machungwa – Tsh. 10,000, VIP C – Tsh. 20,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP A – Tsh. 40,000 na Platinum – Tsh. 150,000.”- Ahmed Ally.

Leave A Reply