The House of Favourite Newspapers

AIKA : MIAKA 10 YA MAPENZI YETU KAMA 2 TU !

Image result for Navy Kenzo
Aika Mariale na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’

Mwanamama kutoka Bongo Flevani, ambaye ni memba wa Kundi la Navy Kenzo, Aika Mariale amesema miaka 10 waliyoishi ya kimapenzi na mzazi mwenzake, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ anaona ni kama juzi tu au miaka miwili.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Aika alifunguka kwamba ndani ya miaka hiyo waliyoishi pamoja kama marafiki wakubwa, wapenzi na watu wanaosi-kilizana, imeweza kuwafundisha vitu vingi kwa sababu wamepitia changamoto nyingi hadi kufika hapo.

“Ulishawahi kukaa na mtu miaka 10, lakini unaona ni kama jana tu? Hii ni kutokana na jinsi mlivyoishi katika upendo na urafiki mkubwa, ndivyo tulivyo mimi na Nahreel na tunaunganishwa zaidi na mtoto wetu, Gold,” alisema Aika

IMELDA MTEMA

Comments are closed.